Mbarali
Wilaya ya Mbarali ni wilaya mojawapo kati ya 7 za Mkoa wa Mbeya. Wilaya hiyo ilianzishwa mnamo mwaka 2000.
Upande wa Kaskazini Mashariki inapakana na Wilaya ya Iringa Vijijini, upande wa Mashariki inapakana na Wilaya ya Njombe, upande wa Kusini inapakana na wilaya ya Mbeya na Kaskazini na Wilaya ya Chunya.
Wakazi
[hariri | hariri chanzo]Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 234,908 [1]. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 446,336 [2].
Makabila makuu yaliyopo wilayani Mbarali ni Wasangu, Wahehe, Wakinga, Wabena na Wanyakyusa. Vilevile yapo makundi madogo ya makabila kama Wasukuma, Wawanji, Wabarbaig na Wagogo.
Makundi mengi ya makabila haya ni wakulima na wafugaji ambao walihamia bonde la Usangu kutoka Mikoa ya Arusha, Mwanza, Shinyanga, Singida na Dodoma.
Eneo
[hariri | hariri chanzo]Eneo lake ni kilometa za mraba 16,000. Katika eneo hili ardhi kwa ajili ya kilimo ni asilimia 20, eneo la wanyama pori takriban 30 %, hifadhi za misitu 1%, maeneo ya makazi mnamo 38% na maeneo ya pori tariban 16%.
Wilaya ya Mbarali iko hasa tambarare ya chini katika Bonde la Ufa. Maji hutelemka kutoka milima na mitelemko ya kando na kukusanyika hapa hivyo wilaya ni a chanzo kikuu cha maji ambacho ni mto Ruaha Mkuu na kuelekea mto Rufiji, halafu Bahari Hindi.
Ekolojia
[hariri | hariri chanzo]Kunda kanda tatu za kiekolojia ambazo ni:
- Uwanda wa Msangaji katika kaskazini una udongo mwenye rutba kidogo, unapokea mvua mm 500 - 900 kwa mwaka na ni sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
- Uwanda wa kati wa Usangu una udongo mweusi na kichanga, unapokea mvua mm 450-650 kwa mwaka ukitumiwa kwa kilimo cha mtama, uwele, mahindi, mpunga na kwa ufugaji.
- Tambarare za Kusini mwa Usangu. Hapa mvua ni haba, mm 360-750. Kilimo ni cha mahindi, karanga, pamba, kilimo cha umwagiliaji cha mpunga halafu ufugaji.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Mbarali (tovuti rasmi ya Mkoa wa Mbeya Ilihifadhiwa 17 Novemba 2016 kwenye Wayback Machine.
Kata za Wilaya ya Mbarali – Mkoa wa Mbeya - Tanzania | ||
---|---|---|
Chimala | Igava | Igurusi | Ihahi | Imalilo Songwe | Ipwani | Itamboleo | Kongolo | Lugelele | Luhanga | Madibira | Mahongole | Mapogoro | Mawindi | Miyombweni | Mwatenga | Ruiwa | Rujewa | Ubaruku | Utengule Usangu |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mbarali kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |