Rujewa
Kata ya Rujewa | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Mbeya |
Wilaya | Mbarali |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 29,473 |
Rujewa ni jina la kata ya Wilaya ya Mbarali katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania. Wakati wa wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 29,473 [1] walioishi humo. Msimbo wa posta ni 53601.
Rujewa iko katika tambarare ya Usangu ambvako maji ya mito kutoka milima ya jirani yanakusanyika na kuwa chanzo cha Mto Ruaha. Hivyo eneo latumiwa kwa kilimo cha umwagiliaji.
Historia ya Rujewa[hariri | hariri chanzo]
Jina Rujewa linatokana na mtu mmoja wa kwanza kuishi Rujewa aliyeitwa Mjewa, aliyekuwepo miaka mingi na familia yake wakaitwa Wajewa ndio hata leo hii pakaitwa Rujewa.
Watwala wa jadi[hariri | hariri chanzo]
Kwa kuwa wenyeji wa mwanzo hapa Rujewa walikuwa Wasangu walikuwa na mtawala wao wa jadi aliyeitwa Chifu Merere.
Uchumi[hariri | hariri chanzo]
Rujewa ni maarufu kwa kilimo cha mpunga hasa ukiangalia Rujewa ndiko yaliko mashamba ya Mbarali Estate na mashamba ya mpunga ya kule Kapunga, lakini pia wenyeji wa Rujewa ni Wasangu, Wabena, Wakinga na hata kuna Waburushi kutoka Pakistan ambao wamekuwa nao ni wenyeji hasa wa Rujewa kwani hufanya shughuli kwa kushilikiana na wenyeji wa Rujewa,
Rujewa inasifika kwa kutoa mchele mzuri kuliko eneo lolote la Tanzania, na baadhi ya mazao ya biashara yanayolimwa Rujewa ni kama alizeti. Pia Rujewa inastawi mazao mengi ya chakula kama vile karanga, mahindi, ulezi nk.
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Sensa ya 2012, Mbeya - Mbarali DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2017-03-14.
![]() |
Kata za Wilaya ya Mbarali – Mkoa wa Mbeya - Tanzania | ![]() |
---|---|---|
Chimala | Igava | Igurusi | Ihahi | Imalilo Songwe | Ipwani | Itamboleo | Kongolo | Lugelele | Luhanga | Madibira | Mahongole | Mapogoro | Mawindi | Miyombweni | Mwatenga | Ruiwa | Rujewa | Ubaruku | Utengule Usangu |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Rujewa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |