Wilaya ya Momba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Momba ni wilaya katika mkoa wa Songwe, ambayo ilianzishwa rasmi mnamo Machi 2012 ikigawiwa toka wilaya ya Mbozi.

Makao makuu ya wilaya yako Chitete, ingawa ofisi zake kwa muda zipo Ukwile katika majengo ya kukodi ya ADP.

Vijiji vinavyozunguka makao makuu ya wilaya ni: Tindingoma, Nkala, Naming'ongo na Yala. Vyote hivyo vipo ndani ya Tarafa ya Msangano.

Mbunge wake anaitwa Silinde kutoka chama cha Chadema.

Lugha kuu zinazozungumzwa ni pamoja na Kinyamwanga na Kiwanda upande wa Tarafa ya Kamsamba.

Mazao yanayolimwa ni mpunga, mahindi, mtama, ufuta, ulezi, alizeti na kahawa.

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Momba - Mkoa wa Songwe - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Chilulumo | Chitete | Chiwezi | Ivuna | Kamsamba | Kapele | Mkomba | Mkulwe | Mpapa | Msangano | Myunga | Ndalambo | Nkangamo | Nzoka


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Songwe bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Momba kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari .
Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno