Tukuyu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Tukuyu
Tukuyu is located in Tanzania
Tukuyu
Tukuyu
Mahali pa mji wa Tukuyu katika Tanzania
Majiranukta: 9°15′0″S 33°38′24″E / 9.25°S 33.64°E / -9.25; 33.64
Nchi Tanzania
Mkoa Mbeya
Wilaya Rungwe

Tukuyu ni mji mdogo na makao makuu ya wilaya ya Rungwe katika mkoa wa Mbeya, Tanzania.

Iko mita 1300 juu ya UB, karibu na mlima wa Rungwe ikitazama beseni la Ziwa Nyasa.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Tukuyu ilianzishwa wakati wa ukoloni wa Kijerumani ikaitwa Neu Langenburg ("boma ndefu mpya") badala ya Langenburg ya awali iliyokaa mwambaoni mwa Ziwa Nyasa ikazama chini wakati wa maji ya ziwa kupanda. Hadi leo jina la hoteli "Langiboss" inakumbuka jina la zamani.

Neu Langenburg ilikuwa mji mkuu wa Mkoa wa Langenburg (takriban mikoa ya Mbeya na Songwe ya leo).

Wakati wa Waingereza ikapewa jina la Tukuyu ikawa mji mkuu wa wilaya.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Tukuyu iko katika eneo lenye mvua nyingi na rutuba; ni kitovu cha kilimo cha chai nchini Tanzania.

Pia ni kitovu cha kilimo cha ndizi za kuiva: takribani mkoa wote wa Mbeya hutegemea ndizi kutoka Tukuyu.

Kwa miaka mingi Tukuyu ilikuwa na tatizo la mawasiliano mabaya kutokana na uharibifu wa barabara pamoja na matatizo ya kisiasa kati ya Malawi na Tanzania.

Siku hizi barabara ni nzuri kuelekea Malawi, pia kwenda Mbeya na Daressalaam.

Kuna nafasi nzuri ya utalii kwa sababu ya uzuri wa mazingira, lakini huduma bado ni chache.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Tukuyu ni eneo la Konde au Wanyakyusa. Mji wenyewe umekuwa kituo cha dayosisi ya Konde ya Walutheri pia dayosisi ya Wakatoliki. Makao makuu ya Moravian bado yako Rungwe misioni.

Taasisi[hariri | hariri chanzo]

Tukuyu ina shule za msingi na sekondari, chuo cha ualimu na taasisi ya utafiti wa tiba, pia kuna ofisi za serikali ambayo ndiyo makao makuu ya Wilaya ya Rungwe (halmashauri) au umma pamoja na mashirika binafsi au taasisi binafsi, pia kuna huduma za posta, smu, hospitali ya wilaya na huduma za benki mbalimbali.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tukuyu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.