Masoko (Rungwe)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Masoko ni kata ya wilaya ya Rungwe katika Tanzania kusini-magharibi. Idadi ya wakazi ni 8,224 (sensa 1999).

Masoko iko kilomita 14 upande wa kusini-mashariki ya Tukuyu kando la ziwa la volkeno.

Kwenye kitovu cha Masoko kuna majengo ya boma ya kihistoria ya zamani ya ukoloni wa Kijerumani. Masoko ilikuwa makao makuu ya kikosi cha tano cha jeshi la ulinzi la koloni.

Wajerumani walipoondoka Masoko mnamo mwaka 1917 wakati wa Vita Kuu ya Dunia ya Kwanza walitupa vitu ziwani na watoto wamechukua mara kwa mara sarafu kutoka ziwani na kuziuza hasa sarafu za heller.

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Rungwe - Mkoa wa Mbeya - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Bagamoyo (Rungwe) | Bujela | Bulyaga | Ikuti | Ilima | Isongole | Katumba | Kinyala | Kisiba | Kisondela | Kiwira | Kyimo | Lufingo | Malindo | Masoko (Rungwe) | Masukulu | Mpuguso | Nkunga | Rufiryo | Suma