Nenda kwa yaliyomo

Hela

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Heller)

Hela ni jina kwa pesa lililo kawaida katika Tanzania. Asili ya neno ni lugha ya Kijerumani. "Heller" ilikuwa kitengo cha pesa ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani au Tanzania bara kuanzia 1904 hadi 1918. Waingereza baada ya kuchukua utawala wa koloni walibadilisha sarafu kuwa shilingi na senti lakini jina la "hela" lilibaki kwa ajili ya pesa kwa jumla.

Heller ya 1913 (mbele)
Heller ya 1913 (nyuma)

Heller ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani

[hariri | hariri chanzo]

Tangu 1904 serikali ya Ujerumani ilichukua wajibu wa kutoa pesa kwa koloni yake katika Afrika ya Mashariki iliyojumlisha Tanzania bara pamoja na Rwanda na Burundi. Hadi mwaka ule Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki iliendelea kutoa sarafu yake iliyokuwa rupie 1 yenye pesa 64. Serikali ilipochukua jukumu hii iliamua kuendelea na rupie lakini ilibadilisha vitengo vyake vidogo kuwa Heller 100. Heller iliwahi kuwa pesa ndogo ya kihistoria katika Ujerumani lakini haikutumiwa tena tangu maungano ya Ujerumani mwaka 1871 na kuanzishwa kwa pesa ya kitaifa ya Mark na Pfennig.

Sarufi za Heller za Afrika ya Mashariki zilionyesha upande wa mbele neno "Heller" na namba ya thamani yake; upande wa nyumba ilikuwa na taji la Kaisari, maneno ya "Deutsch Ostafrika" (Afrika ya Mashariki ya Kijerumani) na mwaka wa kutolewa.

Heller ya Afrika ya Mashariki ilitolewa kwa sarufi za

Heller za Ulaya

[hariri | hariri chanzo]

Asili ya pesa iliyoitwa "heller" ni mji wa Kijerumani wa Hall inayoitwa leo Schwäbisch Hall. Kule sarafu za fedha zilitolewa tangu mwaka 1288 zilizosambaa haraka zikaitwa "Haller" au "Heller" kutokana na jina la mji. Polepole kiasi cha fedha ndani ya sarafu kilipungukiwa hadi kuwa sarafu ya shaba yenye thamani ndogo.

Heller iliendelea kuwa sarafu ndogo ya kawaida (kama senti) katika Ujerumani hadi mwaka 1873 ilipofutwa baada ya kuanzishwa kwa fedha mpya ya Mark na Pfennig. Austria-Hungaria iliendelea kuitumia kama sarafu ndogo ya Krone hadi mwisho wa dola hili. Chekoslovakia kama nchi mojawapo iliyotokana na Austria-Hungaria ilikuwa nchi ya pekee kuendelea na sarafu hii kwa jina "haler". Baada ya kugawiwa kwa Chekoslovakia kuwa nchi mbili za Ucheki na Slovakia zote mbili zilkuwa na haler hadi kujiunga na Euro.