Kinyala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kinyala ni jina la kata ya Wilaya ya Rungwe katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania. Wakati wa wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,871 [1] walioishi humo. Msimbo wa posta ni 53535.

Kinyala inakaliwa na makabila makubwa mawili ambayo ni Wanyakyusa na Wasafwa.

Kata ya Kinyala ina shule 13 za msingi ambazo ni Igogwe, Lukata, Kakala, Isumba, Igembe, Kipande, Songwe, Ikukisya, Kisoko, Swaya, Isebelo, Malangali na Ishinga. Kuna pia shule za sekondari 3 ambazo ni Kinyala na Ziwa Ngosi ambazo ni za serikali na sekondari ya binafsi ya Lubala.

Kwa upande wa afya pia kuna hospitali kubwa moja ya Igogwe Hospital inayomilikiwa na Kanisa Katoliki parokia ya Igogwe.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya 2012, Mbeya - Rungwe DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-03-13.
Kata za Wilaya ya Rungwe - Mkoa wa Mbeya - Tanzania

Bagamoyo | Bujela | Bulyaga | Ibighi | Ikama | Ikuti | Ilima | Iponjola | Isongole | Itagata | Kawetele | Kikole | Kinyala | Kisiba | Kisondela | Kiwira | Kyimo | Lufingo | Lupepo | Makandana | Malindo | Masebe | Masoko | Masukulu | Matwebe | Mpuguso | Msasani | Ndanto | Nkunga | Suma | Swaya


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kinyala kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.