Nenda kwa yaliyomo

Lumbila

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Kata ya Lumbila
Nchi Tanzania
Mkoa Njombe
Wilaya Ludewa
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 2,038
Mahali pa Lumbila kwenye Ziwa Nyasa

Lumbila ni kata ya Wilaya ya Ludewa katika Mkoa wa Njombe, Tanzania. Msimbo wa posta ni 59406.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 2,038 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 1,880 [2] walioishi humo.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa kuanzishwa kwa koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kituo cha Langenburg kilianzishwa hapa mwaka 1893 kando ya mdomo wa mto Luyangala (Wajerumani waliandika "Rumbira"). Langenburg ilikuwa makao makuu ya serikali kwa sehemu za kusini za koloni kwa sababu usafiri ulipatikana kwa njia ya maji tu, ilhali Wajerumani hawakusimamia bado njia za ndani hadi kukandamizwa kwa upinzani wa Wahehe mnamo mwaka 1898 (kifo cha Mkwawa).

Langenburg ilikuwa na boma imara na kituo cha meli ndogo "Hermann von Wissmann" yenye tani 50 iliyokuwa chombo kikuu cha usafiri cha Wajerumani kwenye Ziwa Nyasa na kuzunguka baina ya Langenburg, Wiedhafen (Manda), Fort Johnston (Mangoche, Malawi), Monkey Bay na vituo vingine upande wa Kiingereza wa ziwa.[3]

Mwanzoni Langenburg ilikuwa makao makuu ya Mkoa wa Langenburg lakini baadaye ofisi zilihamishwa katika eneo la Unyakyusa ambako mji mpya ya Neu Langenburg (leo: Tukuyu) ulianzishwa. Kwa kuitofautisha miji miwili jina la Alt-Langenburg ilikuwa kawaida kwa kituo cha kwanza, yaani Lumbila.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.nbs.go.tz, uk 210
  2. "Sensa ya 2012, Njombe - Ludewa DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-03-16.
  3. Linganisha Rudolf Pfitzner, Deutsches Kolonial-Handbuch, Band I, Berlin 1901, uk. 338f (online hapa kwenye archive.org)
Kata za Wilaya ya Ludewa - Mkoa wa Njombe - Tanzania

Ibumi | Iwela | Kilondo | Lifuma | Luana | Lubonde | Ludende | Ludewa | Lugarawa | Luilo | Lumbila | Lupanga | Lupingu | Madilu | Madope | Makonde | Manda | Masasi | Mavanga | Mawengi | Milo | Mkongobaki | Mlangali | Mundindi | Nkomang'ombe | Ruhuhu


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Lumbila kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.