Rungwe (wilaya)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mahali pa Rungwe (kijani) katika mkoa wa Mbeya.
Daraja la Mungu ni kati ya maajabu asilia ya wilaya hii (picha ya Tamino Boehm)

Wilaya ya Rungwe ni kati ya wilaya 8 za Mkoa wa Mbeya katika Tanzania. Imepakana na Wilaya ya Mbeya vijijini upande wa kaskazini, Mkoa wa Iringa upande wa mashariki, Wilaya ya Kyela upande wa kusini-mashariki, Wilaya ya Ileje kwa kusini-magharibi na Mbeya Mjini kwa magharibi. Makao makuu ya wilaya yako Tukuyu.

Mwaka 2002 wilaya ilikuwa na wakazi 307,270.[1] Rungwe ni hasa eneo la Wanyakyusa ikishika sehemu kubwa ya eneo la Unyakyusa lililoitwa kihistoria pia "Konde". Jina la wilaya limetokana na kituo cha misioni ya Moravian cha Rungwe kilichopo kwenye mitelemko ya mlima wa Rungwe takriban 20 km kutoka Tukuyu.

Kati ya mazao ya sokoni kuna mashamba makubwa ya chai. Rungwe inapokea mvua nyingi iko kati ya maeneo yenye rutba sana katika Tanzania.

Barabara kuu kutoka Daressalaam - Iringa - Mbeya kwenda Malawi inapita eneo la wilaya.

Kata[hariri | hariri chanzo]

Wilaya ya Rungwe ina kata 30:

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Sources[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Rungwe - Mkoa wa Mbeya - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Bagamoyo (Rungwe) | Bujela | Bulyaga | Ikuti | Ilima | Isange | Isongole | Itete | Kabula | Kambasegela | Kandete | Katumba | Kinyala | Kisegese | Kisiba | Kisondela | Kiwira | Kyimo | Lufingo | Lupata | Luteba | Lwangwa | Malindo | Masoko | Masukulu | Mpombo | Mpuguso | Nkunga | Rufiryo | Suma |


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rungwe (wilaya) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.