Wilaya ya Ileje

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Ileje (kijani) katika mkoa wa Mbeya.

Wilaya ya Ileje ni wilaya mojawapo kati ya 5 za Mkoa wa Songwe; hadi 2016 ilikuwa sehemu ya Mkoa wa Mbeya.

Wilaya hii imepakana na nchi ya Malawi na inatenganishwa nayo na mto Songwe.

Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 124,450 [1]. Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 125,869 [1].

Wenyeji wa Ileje ni wenye asili ya makabila matatu, yaani Wandali, Walambya na Wamalila (Ibaba, Itale).

Kama ilivyo kwa mkoa mzima, Ileje kuna wafuasi wengi wa dini ya Ukristo na wachache wa Uislamu.

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Wilaya hii ina kata zifuatazo:

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Ileje - Mkoa wa Songwe - Tanzania

Bupigu | Chitete | Ibaba | Ikinga | Isongole | Itale | Itumba | Kafule | Kalembo | Lubanda | Luswisi | Malangali | Mbebe | Mlale | Ndola | Ngulilo | Ngulugulu | Sange |


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Songwe bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Ileje kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari .
Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno