TANZAM
TANZAM (kifupi cha Tanzania-Zambia-Highway) ni barabara kuu kati ya Dar-es-Salaam (Tanzania) na Lusaka (Zambia).
Sababu za kujengwa kwa TANZAM
[hariri | hariri chanzo]Barabara hiyo ilipanuliwa na kuimarishwa kama barabara ya lami kati ya miaka 1968 hadi 1973. Kusudi lake lilikuwa la kisiasa maana Zambia ilitafuta njia ya mawasiliano na bandari ya baharini bila kutegemea tena Afrika Kusini.
Kihistoria usafiri wa nje na biashara ya Zambia isiyo na pwani vilitegemea njia zilizopita katika Msumbiji au Afrika Kusini na nchi zote mbili hazikuwa bado nchi huru. Msumbiji ilikuwa koloni la Ureno na Afrika Kusini ilitawaliwa na serikali ya Apartheid.
Tanzania ilivutwa na mpango huo kwa sababu ilipinga ukoloni, pia ilitarajia faida za biashara na Zambia, Malawi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Nchi ilikuwa pia na haja ya kuboresha barabara zake na TANZAM inaunganisha pia nyanda za juu za kusini za Tanzania na Dar es Salaam.
TANZAM ndani ya Tanzania
[hariri | hariri chanzo]TANZAM ina urefu wa kilomita 2,400 na zote zina lami. Katika Zambia huitwa Great North Road na ndani ya Tanzania ilikuwa na namba T1. Siku hizi sehemu ya Dar es Salaam - Iringa huitwa A7, na sehemu ya Iringa - Mbeya - Tunduma huitwa A104
Inaanza mjini Dar es Salaam ikipita katika mikoa ya Pwani, Mkoa wa Morogoro!Morogoro, Iringa na Mbeya. Kati ya Dar na Morogora njia inapita katika hifadhi ya Mikumi.
Ndani ya Tanzania ina njiapanda 4 muhimu:
- mjini Chalinze iko chanzo ya barabara kuu inayoelekea Tanga na Kilimanjaro-Nairobi
- mjini Morogoro iko njiapanda ya barabara kwenda Dodoma inayoendelea magharibi hadi Mwanza na Kigoma
- mjini Makambako kuna njiapanda ya barabara kwenda Songea inayoendelea katika hali mbaya hadi Mtwara
- Uyole/Mbeya iko njiapanda ya barabara kwenda Malawi kupitia Tukuyu.
Kuanzia Makambako TANZAM inaendelea mara nyingi kando ya njia ya reli ya TAZARA.
TANZAM ndani ya Zambia
[hariri | hariri chanzo]Mjini Tunduma TANZAM inavuka mpaka na kuingia Zambia. Sasa ni "Great North Road" ikielekea Kapiri Mposhi kupitia Nakonde na huko inapewa namba T2. Kapiri Mposhi inajiunga na barabara kuu ya Zambia kutoka Lumbumbashi (Kongo) kwenda Lusaka.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Historia ya Tanzam en Ilihifadhiwa 17 Juni 2006 kwenye Wayback Machine.