Mkoa wa Pwani


Mkoa wa Pwani ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Umepakana upande wa Kaskazini na mkoa wa Tanga, upande wa mashariki na Dar-es-Salaam na Bahari Hindi, upande wa kusini na mkoa wa Lindi na upande wa magharibi na mkoa wa Morogoro. Mkoa huo una eneo la km² 32,407, na idadi ya wakazi wapatao 2,024,947 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 [1] kutoka 1,098,668 (2012). Mkoa huo ni maarufu kwa shughuli za utalii hususani katika mji wa Bagamoyo, kisiwa cha Mafia na Hifadhi ya Taifa ya Saadani. Makao makuu ya mkoa yako Kibaha.
Wilaya na wakazi
Mkoa wa Pwani una wilaya nane (katika mabano idadi ya wakazi wakati wa sensa ya mwaka 2022 [2]):
- Bagamoyo (205,478)
- Chalinze (316,759)
- Kibaha Mjini (265,360)
- Kibaha Vijijini (123,367)
- Kisarawe (159,226)
- Mkuranga (533,033)
- Mafia (66,180)
- Rufiji (159,906)
- Kibiti (195,638).
Mkoa huo wenyeji wake ni watu wa makabila ya Wakwere, Wazaramo, Wandengereko, Wadoe, Wazigua na Wanyagatwa.
Majimbo ya bunge
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huo ulikuwa na majimbo ya uchaguzi tisa yafuatayo [3]:
- Chalinze : mbunge ni Ridhwan Kikwete (CCM)
- Bagamoyo : mbunge ni Shukuru Kawambwa (CCM)
- Kibaha Mjini : mbunge ni Sylvester Francis Koka (CCM
- Kibaha Vijijini : mbunge ni Hamoud Abuu Jumaa (CCM)
- Kisarawe : mbunge ni Selemani Said Jafo (CCM)
- Mafia : mbunge ni Mbaraka Kitwana Dau (CCM)
- Mkuranga : mbunge ni Abdallah Hamis Ulega (CCM)
- Kibiti : mbunge ni Ally Seif Ungando (CCM)
- Rufiji : mbunge ni Mohamed Omary Mchengerwa (CCM)
Tazama pia
Tanbihi
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-11-07. Iliwekwa mnamo 2022-11-14.
- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ Kuhusu makadirio ya idadi ya watu katika majimbo ya uchaguzi Tanzania Bara kwa mwaka 2016: [http://www.nbs.go.tz/nbs/takwimu/majimbo/MAJIMBOApril_Kisw.pdf
Viungo vya nje
- Tovuti rasmi ya Mkoa wa Pwani, Tanzania
- (Kiingereza) Matokeo ya sensa 2002 kwa ajili ya mkoa wa Pwani
- Habari za Pwani kwenye kurasa za Tume ya Uchagizi Ilihifadhiwa 21 Februari 2006 kwenye Wayback Machine.
| Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi | |