Wilaya ya Mafia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mafia ni moja kati ya wilaya 6 za mkoa wa Pwani katika Tanzania yenye postikodi namba 61700[1]. Eneo lake ni hasa Kisiwa cha Mafia na visiwa vidogo karibu nacho. Mji mkuu na makao makuu ya wilaya ni Kilindoni. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, wilaya ilikuwa na wakazi wapatao 46,438 [2] walioishi humo.

Kata za wilaya ya Mafia ni kama zifuatazo[3]:

Shehia Eneo
km²
Wakazi
2002
Vijiji
Baleni[4] 132.1 9137 Baleni, Kungwi, Ndagoni[5], Chunguruma
Jibondo 21.9 3405 Jibondo, Chole, Juani
Kanga 52.7 3317 Kanga, Bweni
Kilindoni 36.8 11696 Kilindoni, Dongo
Kirongwe 77.0 5260 Kirongwe, Jimbo, Banja, Jojo
Kiegeani 40.3 3379 Kiegani, Marimbani
Miburani 52.3 4363 Miburani, Mlongo, Chemchem
Wilaya ya Mafia 413 40801 20 villages
Tanzania Mafia district wards map.png

Baleni, Kanga na Kirongwe kwa pamoja ni tarafa ya kaskazini, shehia nyingine ni tarafa za kusini.

Wilaya hii inajumuisha funguvisiwa pamoja na kisiwa cha Mafia ndani yake inayotazama mwambao wa Afrika ya Mashariki 130 km kusini ya Daressalaam karibu na mdomo wa Mto Rufiji. Umbali wake na bara ni 16 km.

Mafia kisiwa kikuu ina urefu wa 50 km na upana wa 8 km; eneo lake ni takriban 400 km². Inajulikana pia kwa jina "Chole shamba" kutokana na mji wa kale wa Chole iliyokuwepo kwenye kisiwa kidogo cha Chole mjini karibu na kisiwa kikuu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.tcra.go.tz/images/documents/postcode/pwani.pdf[dead link]
  2. Sensa ya 2012, Pwani - Mafia DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-06-13.
  3. [International Resources Group: Strategic Environmental Assessment of Mafia Island, FINAL REPORT, Volume II: Main Report] (PDF)
  4. Tangu kupatikana kwa orodha hii Baleni imegagiwa na Ndagoni kuwa kata ya pekee
  5. Tangu kupatikana kwa orodha hii Baleni imegagiwa na Ndagoni kuwa kata ya pekee


Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Mafia - Mkoa wa Pwani - Tanzania Flag of Tanzania.svg

BaleniJibondoKangaKiegeaniKirongweKilindoniMiburaniNdagoni