Jibondo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jibondo ni kata ya Wilaya ya Mafia katika Mkoa wa Pwani, Tanzania, yenye postikodi namba 61705.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 4,333 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 3,729 [2] walioishi humo.

Kata ya Jibondo inajumlisha visiwa vidogo vya Juani, Jibondo na Chole. Idadi kubwa ya wakazi wako Jibondo.

Watu hutegemea hasa uvuvi pamoja na kilimo kilichopo hasa Chole. Maji matamu hayapatikani kwenye visiwa hivi: ni lazima kuyabeba kila siku kutoka kisiwa kikuu cha Mafia isipokuwa wakati wa mvua ambako maji ya mvua hukusanywa. Chole imeunganishwa sasa na maji ya bomba kutoka Utende (kata ya Kiegeani) kwenye kisiwa cha Mafia.

Chole na Juani zilikuwa na miji muhimu katika historia ya visiwa hivi. Mji wa Chole kilikuwa mji mkuu wa Mafia yote hadi ukoloni wa Kijerumani. Hadi leo kuna maghofu ya majengo makubwa ya serikali ya kikoloni pamoja na nyumba za wafanyabiashara Waarabu, Waswahili na Wahindi waliokuwa na makampuni 14 pale Chole katika mwaka 1913. Mwaka ule makao makuu ya serikali ilihamishiwa Kilindoni kwenye kisiwa kikuu cha Mafia. Jengo la kituo cha forodha cha Kijerumani limekarabatiwa liko mahali ambako kivuko kutoka Utende - Kiegani kinafika.

Kisiwa cha Juani kina maghofu ya mji wa Kua uliokuwa mji muhimu wa biashara. Asili zake zimethibitishwa hadi karne ya 12 BK.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.nbs.go.tz/
  2. Sensa ya 2012, Pwani - Mafia DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-06-13.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Mafia - Mkoa wa Pwani - Tanzania

BaleniJibondoKangaKiegeaniKirongweKilindoniMiburaniNdagoni


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Pwani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Jibondo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.