Nenda kwa yaliyomo

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ridhwan Kikwete)

Ridhiwani Jakaya Kikwete (amezaliwa 16 Aprili 1979) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa Chama cha kisiasa cha Chama Cha Mapinduzi (CCM). Alichaguliwa tena kuwa mbunge wa Chalinze kwa miaka 20152020. [1]

Ridhiwani ni mtoto wa rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete.

Alianza safari yake ya elimu katika shule ya msingi Matangani mwaka 1987 hadi 1988 na kuhamia Mkomaindo Primary School mwaka 1988 hadi 1989. Hakuishia hapo, alijiunga na shule ya msingi Forodhani mwaka 1990 na kuhitimu mafunzo ya msingi 1993. Alifanikiwa kujiunga na shule ya sekondari ya Shaaban Robert mwaka 1994 na kuhitimu kidato cha nne mwaka 1997. Baadae alijiunga na Mkwawa High School kwa masomo ya kidato cha tano na sita kwanzia mwaka 1998 na kuhitimu mwaka 2000.

Mwaka 2001 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kusoma shahada ya sheria na kuhitimu mwaka 2005. BaadaYe alijiendeleza kimasomo katika chuo cha Hull University [2] huko nchini Uingereza mwaka 2007 hadi 2008. Alisoma Stashahada ya Uzamili ya maendeleo ya biashara.

Amefanya kazi kama mwanasheria katika kampuni mbalimbali, ya kwanza ilikuwa IMMA Advocates mwaka 2005 hadi 2009 na Tanganyika Law Society mwaka 2009 hadi 2016 wakati huohuo akifanya kazi na East Africa Law Society.