Wilaya ya Kibiti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wilaya ya Kibiti ni wilaya mpya katika Mkoa wa Pwani iliyoanzishwa mnamo mwaka 2015 yenye postikodi namba 61800[1]. Maeneo yake yalitengwa na Wilaya ya Rufiji.

Kulingana na matokeo ya sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilikadiriwa kuwa 133,727 kwa mwaka 2016. [2]

Misimbo ya Posta katika wilaya hii huanza kwa namba 616.

Wilaya ya Kibiti inajumlisha ndani yake kata za delta ya mto Rufiji ambazo hazijafikiwa bado na maendeleo ya miundombinu hadi mwaka 2017.

Kata na Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Wilaya ya Kibiti ilikadiriwa kuwa na wakazi 133,727 mnamo mwaka 2016.

Kata zake zilikuwa na wakazi wafuatao:

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.tcra.go.tz/images/documents/postcode/pwani.pdf[dead link]
  2. Makadirio ya idadi ya watu katika majimbo ya uchaguzi Tanzania Bara kwa mwaka 2016, uk. 56; tovuti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu, iliangaliwa Juni 2017

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Kibiti - Mkoa wa Pwani - Tanzania

Bungu | Dimani | Kibiti | Kiongoroni | Mahege | Maparoni | Mbuchi | Mchukwi | Mjawa | Mlanzi | Msala | Mtawanya | Mtunda | Mwambao | Ruaruke | Salale