Wilaya ya Chalinze

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wilaya ya Chalinze ni moja ya wilaya nane za Mkoa wa Pwani, Tanzania. Maeneo yake yalitengwa mwaka 2015 na Wilaya ya Bagamoyo na halmashauri yake ilianza kufanya kazi rasmi mwezi Julai 2016[1]. Makao makuu yapo mjini Chalinze

Eneo la Wilaya ya Chalinze ni km2 8,042 zinazolingana na hekta 804,200. Takribani hekta 404,859 zinatumika kwa shughuli za kilimo na mifugo na hekta 51,127 ni misitu ya hifadhi za vijiji. Hifadhi za Saadani na Wami zinapatikana ndani ya wilaya hiyo. Pamoja na Bagamoyo misimbo ya posta huanza kwa 613.

Wilaya hiyo inapakana na Wilaya za Handeni na Pangani upande wa kaskazini na upande wa kusini na Wilaya za Bagamoyo na Kibaha. Magharibi iko Morogoro Vijijini na upande wa mashariki wilaya inapakana na Bahari ya Hindi.

Barabara muhimu za A7 (TANZAM)]] na A14 zinapita humo zikikutana mjini Chalinze.

Tabianchi ni ya kitropiki na kiwango cha mvua ni kati ya mm 800 hadi 1200 kwa mwaka. Mvua za vuli zinaanza kati ya mwezi Machi hadi katikati ya mwezi Mei. Majira ya kiangazi yanaanza katikati ya mwezi Mei hadi Oktoba.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Historia ya Halmashauri ya Chalinze, tovuti rasmi, iliangaliwa mnamo Septemba 2020
Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Chalinze - Mkoa wa Pwani - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Bwilingu | Kibindu | Kimange | Kiwangwa | Lugoba | Mandera | Mbwewe | Miono | Mkange | Msata | Msoga | Pera | Talawanda | Ubenazomozi | Vigwaza