Wilaya ya Pangani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Wilaya ya Pangani (kijani cheusi) katika Mkoa wa Tanga (kijani) nchini Tanzania

Wilaya ya Pangani ni kati ya wilaya za Mkoa wa Tanga katika Tanzania yenye Postikodi namba 21300.

Imepakana na wilaya ya Muheza upande wa Kaskazini, Wilaya ya Handeni upande wa magharibi, wilaya ya Bagamoyo (Mkoa wa Pwani) upande wa kusini na Bahari Hindi upande wa mashariki. Makao makuu ya wilaya yako Pangani mjini.

Wilaya ina wakazi 54,025 (2012) [1] katika tarafa 4, kata 14 na vijiji 33. Ina shule za msingi 35, shule za sekondari 10 na zahanati 16.[2]

Eneo la wilaya ni kama kanda linalofuata ufuko wa Bahari Hindi. Mji wa Pangani upo mdomoni mwa mto Pangani unaoingia ndani ya nchi kavu kwa umbo la mlango mpana. Maeneo yaliyo karibu zaidi na bahari yenye ardhi ya rutuba kuna kilimo cha korosho, nazi, mihogo, mahindi, viazi vitamu na ndizi. Maeneo ya ndani zaidi pasipo rutuba sana kuna mashamba ya katani na mahindi.

Kihistoria mazingira ya Pangani ni kati ya maeneo ya utamaduni wa Uswahilini; kabla ya ukoloni kulikuwa na mashamba ya Waarabu waliotumia watumwa na tangu kufika kwa ukoloni wa Kijerumani mashamba makubwa ya katani yalianzishwa.

Wilaya hii ilikuwa pia nyumbani ya Abushiri ibn Salim al-Harthi na chanzo cha vita ya Abushiri dhidi ya utawala wa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo na Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

  • Sensa ya 2012, Tanga - Pangani DC[dead link]
  • [1]
  • Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
    Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Pangani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
    Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
    Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
    Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.
    Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Pangani - Mkoa wa Tanga - Tanzania Flag of Tanzania.svg

    Bushiri | Bweni | Kimang'a | Kipumbwi | Madanga | Mkunguni | Mkalamo (Pangani) | Mkwaja | Mwera | Pangani Magharibi | Pangani Mashariki | Tungamaa | Ubangaa