Kata (eneo)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kata ni ngazi ya chini ya utawala wa nchi. Mara nyingi huitwa pia kwa jina lake la Kiingereza kama "ward". Kata ziko chini ya wilaya (district) na kila wilaya huwa na kata kadhaa.

Nchini Tanzania afisa mtendaji wa kata huitwa pia Katibu Kata.

Ndani ya kila kata kuna vijiji au kama ni kata ya mjini kuna mitaa ndani yake.

Ndani ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kata huitwa "shehia".