Wilaya ya Handeni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wilaya za Handeni katika mkoa wa Tanga

Wilaya ya Handeni ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Tanga katika Tanzania.

Imepakana na wilaya ya Kilindi upande wa magharibi, wilaya ya Korogwe na Mkoa wa Kilimanjaro upande wa kaskazini, wilaya ya Pangani upande wa mashariki na Mkoa wa Pwani kwa kusini.

Mwaka 2002 ilikuwa na wakazi 249,572. [1] Iligawiwa katika Wilaya ya Handeni Mjini na Wilaya ya Handeni Vijijini mnamo mwaka 2012. Katika sensa ya mwaka 2022 waliobaki upande wa vijijini walihesabiwa 384,353 [2].

Tarafa[hariri | hariri chanzo]

Wilaya ya Handeni ina tarafa 7: Chanika, Sindeni, Mkumburu, Magamba, Kwamsisi, Mzundu na Mazingara.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Handeni Vijijini - Mkoa wa Tanga - Tanzania

Kabuku | Kabuku Ndani | Kang'ata | Kitumbi | Kiva | Komkonga | Kwachaga | Kwaluguru | Kwamatuku | Kwamgwe | Kwamsisi | Kwankonje | Kwasunga | Kwedizinga | Mazingara | Mgambo | Misima | Mkata | Ndolwa | Segera | Sindeni

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Handeni kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.