Katani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyuzi za katani ya mkonge.
Kiwanda cha katani ya mkonge, maeneo ya Tanga, Afrika ya Mashariki ya Kijerumani mnamo mwaka 1910

Katani ni mmea wenye asili ya Meksiko unaotumika kutengeneza kamba, mikeka, mazulia, vitambaa, gesi na mengineyo.

Katani ililetwa na Dr. Richard Hindorf mwaka 1892 aliyesafirisha miche elfu moja akipitia Florida (Marekani) halafu Hamburg (Ujerumani) ila alipofika Hamburg aligundua amebakiwa na miche mia mbili tu. Hapo alifanya jitihada ya kuitunza miche iliyobaki isiharibike: mpaka alipofika Tanga alikuwa amebakiwa na miche sitini na mbili tu, hivyo aliisafirisha tena mpaka Pangani katika kijiji cha Kikogwe ambapo alianzisha shamba la kwanza la mkonge.

Katani ni hasa nyuzi za mimea hiyo.

Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Katani kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.