Nenda kwa yaliyomo

Richard Hindorf

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha yake kutoka gazeti la 'Afrika Nachricht (Leipzig).

Richard Hindorf (Duisburg - Ruhrort, , Ujerumani, Novemba 17, 1863 - Berlin - Dahlem, Mei 13, 1954) alikuwa mwanasayansi Mjerumani wa kilimo, na msafiri. Alishughulika sana na Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (kwa Kijerumani: Deutsch-Ostafrika) katika maisha yake.

Baba yake, Heinrich, alikuwa mwalimu wa shule. Baada ya kumaliza shule, alifika Halle kusoma kilimo na sayansi ya siasa. Halafu, akafanya kazi huko New Guinea, ambako alisimamia kituo kikuu cha mashamba ya Kampuni ya New Guinea kutoka 1887 hadi 1889.

Kwa hamu ya kuona nchi za wakoloni alitembea mpaka Java, Sumatra, Australia, Ceylon na Misri .

Afrika Mashariki ya Ujerumani

[hariri | hariri chanzo]

Alifika Afrika Mashariki ya Ujerumani mwaka wa 1891, na baadaye, alirudi nchini mara kwa mara katika maisha yake. Awali, alianza shamba la kahawa hapo Derema, penye milima ya Usambara. Pia alitoka kwenda safari ya Afrika Kusini Magharibi mwa Afrika (Kijerumani: Deutsch-Südwestafrika ), Afrika Kusini, Msumbiji na Kamerun. [1]

Mchango wake muhimu wa kilimo katika Afrika Mashariki ulikuwa kuanzisha kilimo cha mkonge, hasa katika eneo la Usambara na Tanga. Miaka ya 1892-3, alisoma katika Bulletin ya Kew namba 62 kwamba mmea wa mkonge, Agave sisalana, ambao hupatikana nchini Mexico, unaweza kusitawi katika mazingira ya hali ya hewa sawa na Mexico, na alijaribu kupanda mkonge wa kwanza ulioletwa kutoka Florida, karibu na mdomo wa Mto Pangani. [2] Mafanikio yasiyofikirika ya mashamba ya mkonge mwishowe yalisababisha bidhaa hiyo kuwa mkuu wa nchi kuuza nje kwa miaka mingi na chanzo kubwa cha mapato kwa uchumi. Hatimaye, Tanganyika ikawa muuzaji mkubwa wa mkonge kuliko nchi zote nyingine duniani. [3]

Mashamba ya mkonge huko Mlima Uluguru

Mchango mwingine muhimu ulikuwa katika msingi wa Taasisi ya Utafiti ya Amani. Hata mwaka wa 1890, katika gazeti la Kijerumani, [4] alileta wazo la kituo cha utafiti katika koloni ya Afrika Mashariki ya Ujerumani kama vituo vingine vilivyosimamishwa katika koloni za Uingereza na Uholanzi.

Azimio la kuimarisha kituo cha utafiti kitropiki katika Afrika Mashariki ya Ujerumani 1898

Hindorf mwenyewe alikuwa mshiriki mwenza wa Kamati ya Uchumi ya Kikoloni (Kijerumani: Kolonial-wirtschaftliches Komitee ), na kamati hiyo mwaka wa 1898 ilisanya fedha huko Berlin kwa lengo la kuanza na kuendesha kituo hicho cha utafiti kitropiki katika milima ya Usambara. [5] Kwa msaada wa Franz Stuhlmann, mwanabotania Mjerumani, kituo hicho kilijengwa huko Amani, Wilaya ya Muheza, katika milima ya Usambara Magharibi, pamoja na bustani kubwa ya mimea na miti.

Wakati wa Vita vya Kwanza vya Ulimwengu, mwaka wa 1915, aliingia vitani katika jeshi chini ya Paul von Lettow-Vorbeck, na alishiriki katika upinzani maarufu wa askari wa Ujerumani katika ukoloni huo mpaka mwisho. Hata hivyo, alikamatwa na Uingereza huko Dar es salaam mwaka wa 1917 na alifungwa gerezani. [6]

Machapisho

[hariri | hariri chanzo]
  • Maandiko ya kuhusiana na Richard Hindorf katika Maktaba ya Kitaifa ya Ujerumani [7]
  • Wasifu wa Hindorf, Richard katika Deutsche Biographie [8]
  1. Berliner-Börsen Zeitung 17th Nov 1943 ? Richard Hindorf at http://webopac.hwwa.de/PresseMappe20/PM20.cfm?T=P&qt=150432&CFID=47244050&CFTOKEN=55659833 Ilihifadhiwa 10 Julai 2021 kwenye Wayback Machine.
  2. Tanganyika Standard 14th Aug 1937 ?Richard Hindorf at http://webopac.hwwa.de/PresseMappe20/PM20.cfm?T=P&qt=150432&CFID=47244050&CFTOKEN=55659833 Ilihifadhiwa 10 Julai 2021 kwenye Wayback Machine.
  3. 'Britannica' https://www.britannica.com/place/Tanzania/German-East-Africa#ref419185
  4. Kolonialbibliothek 'Deutsche Kolnial Zeitung' No 21 http://sammlungen.ub.uni-frankfurt.de/kolonialbibliothek/periodical/titleinfo/7735725
  5. 'Eine Versuchsstation für Tropenkulturen in Usambara', Hindorf, Richard; Warburg, Otto Berlin : Kolonial-wirtschaftliches Komitee, 1898.
  6. Nachrichten über Dr. Hindorf Gefangennahme durch die Engländer in Ostafrika (111924) Kriegsmitteilungen des Kolonial Wirtschaftlichen Komitees (Berlin), Nr. 24 http://webopac.hwwa.de/PresseMappe20/DigiView_NxtPrv2.cfm?&at=163322&CFID=47199031&CFTOKEN=61770970 Ilihifadhiwa 9 Julai 2021 kwenye Wayback Machine.
  7. https://portal.dnb.de/opac.htm?method=simpleSearch&query=124340679
  8. https://www.deutsche-biographie.de/gnd124340679.html#ndbcontent