Wilaya ya Muheza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muheza

Wilaya ya Muheza ni kati ya wilaya 10 za Mkoa wa Tanga katika Tanzania yenye Postikodi namba 21400. Makao makuu yapo mjini Muheza.

Mwaka 2012 ilikuwa na wakazi 204,461 [1] wanaoishi katika kata 33 za wilaya hiyo.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Muheza ni moja ya wilaya inayopatikana mkoani Tanga. Ukiwa katika wilaya hii unapata kufika kwenye mitaa na maeneo kama Magila (Mbwego), maeneo kama Mkuzi, maeneo kama Bwembera na maeneo kama Tongwe. Vilevile maeneo kama Misozwe, Mkinga, Mkuzi, Moa, Mtimbwane, Mtindiro Mwakijembe, Ngomeni, Nkumba, Pande, Potwe, Songa, Tingeni, Zirai, Mkumbi na Enzi. Wilaya ya Muheza ina ukubwa wa eneo linakadiliwa kufikia zaidi kilomita za mraba 1470. Wilaya hii ilianzishwa mnamo mwaka 1994 na kuwa moja ya wilaya nane zinazopatikana mkoani Tanga. kama ilivyo kwa wilaya zingine za mkoa wa Tanga, Wilaya hii ina historia kubwa sana na ya kipekee. Wakazi wanaopatikana kwenye wilaya hii ni Wabondei (Wa-Mabondeni). Kama inavyoelezwa na baadhi ya wanahistoria kama wakina Nkondokaya, kuwa wakazi wa mwazo kabla ya ujio wa Wabondei, walikuwa Wandorobo waliokuwa wakiishi kwa kuwinda na kuokotaokota. Lakini miaka ya 1700, wakati Wazigua wanafika maeneo ya Ukilindi (kilimani), waliweza kugawanyika na kusambaa kwenye maeneo ya Muheza ambako ndiko leo wako Wabondei. Na hivyo mji wa Muheza kuwa makazi ya asilia kwa Wabondei. Kwa upande Wageni, wageni wa kwanza kufika maeneo hayo ya Muheza walikuwa Waarabu ambao walikuja kufanya biashara na wakazi wa maeneo hayo kuanzia miaka ya 1800. Licha ya kwamba Waarabu walifika Afrika Mashariki tangu miaka ya 700 BK, mahusianao yao ya kibiashara yalikuja kukuwa kipindi cha miaka ya 1800. Hasa kile kipindi ambacho utawala wa Oman ulihamia kisiwani Zanzibar. Hivyo mji wa Muheza ukawa moja ya mji uliopata kukua tangu miaka hiyo. Wageni wa pili kufika kwenye maeneo hayo ya Muheza, ni wageni kutoka Ulaya. Kwanza kulikuwa na Wareno ambao walipata kufika maeneo hayo kwenye miaka ya 1490. Ambao walikuwa walitawala maeneo ya Afrika mashariki, kuaondoshwa mnamo miaka ya 1690. Wageni wengine kutoka Ulaya walikuja kuanzia miaka ya 1840/1850, ambao ni Wamishionari na mfano mzuri wa wamishionari ni Krapf na Rebmann. Na mpaka kufikia miaka ya 1890, kipindi ambacho ukoloni unaanza barani Afrika. Tanganyika ilikabidhiwa kwa Wajerumani na baadhi ya ardhi (maili kupewa Sultani wa Zanzibar). Muheza palikuwa moja ya maeneo ambayo wakoloni waliweza kuanzisha mashamba na shughuri zingine za kidini. Kipindi cha kudai Uhuru maeneo ya Muheza na Tanga kwa ujumla ni moja ya maeneo ambayo wana TANU walikumbana na changamoto nyingi sana. Changamoto zilitoka kwa watawala wa kikoloni wakati huo Waingereza na hata baadhi ya Viongozi wa makabila yaliokuwa yakipatikana Mheza na Tanga kwa wakati huo. Na mara baada ya uhuru Muheza ilikuwa miongoni mwa majimbo. Na mpaka kufikia mwaka 1994 jimbo la Muheza lilikuja kuwa Wilaya.

Asili ya jina[hariri | hariri chanzo]

Asili ya jina muheza linahusiana sana na Wabondei. Inasimuliwa na baadhi ya wazee na wanahistoria kuwa, asili ya jina Muheza ni neno “Mheza”. Na masimulizi yanadai kuwa kulikuwa na vita kati ya Wabondei na Wadigo. Vita hivyo vilitokana na wale Wazigua waliokimbilia na kufika maeneo ya pwani ya Tanga wakitokea maeneo ya Ukilindi na ndio hao Wabondei. Ambapo mapambano yao yalianza pwani ya Tanga na kufika maeneo ya Muheza ya leo. Wabondei wakiwa pwani ya Tanga walionekna kuzidiwa na hivyo waliamua kukimbilia maeneo hayo ya Muheza na walipofika hapo walisema “Hanu Mheza” ikiwa na maana kuwa hapa mmekwisha. Na ndipo Wadigo walipopigwa na Wabondei na kukimbilia maeneo ya Tanga mjini na maeneo yale kukaliwa na Wabondei. Wabondei wao walipaita Mheza lakini baadaye matamshi ya waswahili na wageni wengine waliweza kuweka matamshi mapya na kupata jina Muheza.[2]


Marejeoe[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya 2012, Tanga - Muheza DC[dead link]
  2. Na Mwalimu Joseph Mayuni kama jinsi alivyofanya uchambuzi kuhusu "Muheza" kwa kutumia vitabu vya Nkondokaya. G (2003) Historia ya Waseuta na Abdallah. H. B. (2003) Dola Kongwe Ya Zanzibar.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Muheza kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.
Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Muheza - Mkoa wa Tanga - Tanzania
Flag of Tanzania.svg

Amani | Bwembwera | Genge | Kicheba | Kigombe | Kilulu | Kisiwani | Kwabada | Kwafungo | Kwakifua | Kwemingoji | Kwemkabala | Kwezitu | Lusanga | Magila | Magoroto | Majengo | Makole | Masuguru | Mbaramo | Mbomole | Mhamba | Misalai | Misozwe | Mkuzi | Mlingano | Mpapayu | Mtindiro | Ngomeni | Nkumba | Pande Darajani | Potwe | Songa | Tanganyika | Tingeni | Tongwe | Zirai