Zulia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Zulia aina ya Ardabil
Zulia dogo

Zulia ni aina ya kitambaa kinene ambacho mara nyingi hutumiwa kufunika sakafu.

Mazulia hutumiwa kwa madhumuni mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuhami miguu ya mtu kutoka kwenye ubaridi wa sakafu ya saruji, kufanya chumba kuwa kizuri zaidi kama mahali pa kukaa sakafu (kwa mfano, wakati wa kucheza na watoto au kama mahali pa sala), kupunguza sauti ya kutembea (hasa katika majengo ya ghorofa) na kuongeza mapambo au rangi kwenye chumba. Mazulia hutengenezwa kwa rangi yoyote kwa kutumia nyuzi tofauti za rangi. Kuanzia miaka ya 2000, mazulia yanatumiwa pia katika viwanda, maduka ya rejareja na hoteli.

Inaaminiwa kuwa mazulia yalianza kutumika karne ya 3 au 2 KK huko Asia ya Magharibi, labda eneo la Bahari ya Kaspi (Irani ya kaskazini) au Miinuko ya Armenia. Zulia zee kabisa duniani ni zulia la Pazyryk[1] ambalo ni la karne ya 5 KK. Zulia hili lilifukuliwa na Sergei Ivanovich Rudenko mwaka wa 1949 kutoka kwenye milima Altai huko Siberia.

Zulia la Pazyryk ndio zulia zee kuliko yote duniani. Linatoka (Armenia karne ya 5 KK.)

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "The State Hermitage Museum: Collection Highlights". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-10-05. Iliwekwa mnamo 2017-11-07. 

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zulia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.