Ardabil

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ardabil ikitazamwa kutoka mlimani
Kaburi la Sheikh Safi

Ardabil (pia Ardabīl na Ardebīl , Kiajemi na Kiazeri : اردبیل) ni mji wa kihistoria kaskazini-magharibi mwa Iran. Jina Ardabil linatokana na jina la Kiajemi cha kale "Artawila", likimaanisha mahali patakatifu. [1] Ardabil ni makao makuu wa Mkoa wa Ardabil . Katika sensa ya 2011, idadi ya wakazi ilikuwa 564,365 katika familia 156,324, Wakazi wengi ni Waazeri. [2] [3] Ardabil pia inajulikana kwa patakatifu na kaburi la Safî ad-Dîn na jina lake lilikuwa chanzo cha nasaba ya wafalme wa Safavi .

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Iranian Provinces: Ardabil
  2. "Ardabil". Looklex Encyclopaedia. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-09-28. Iliwekwa mnamo 2013-08-13. 
  3. "Ardabīl". Encyclopædia Britannica. Iliwekwa mnamo 2013-08-13. 

Tovuti za Nje[hariri | hariri chanzo]