Kipumbwi
Kipumbwi ni kata ya Wilaya ya Pangani katika Mkoa wa Tanga, Tanzania yenye Postikodi namba 21311. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ina wakazi wapatao 3,876 [1] waishio humo.
Kata hii ina vitongoji vinne ambavyo ni Serewani, Kipumwbwi Mtoni na Kipumbwi Mji Mpya.
Katika kata ya Kipumbwi, shughuli kubwa ya uchumi ni uvuvi. Wakazi wa Kipumbwi hujishughulisha na shughuli kadhaa za uzalishaji mali kama vile uvuvi, kilimo, biashara na usafirishaji.
Kipumbwi ni jina la kale kidogo kwenye pwani ya Uswahilini; wakati wa karne ya 19 Kipumbwi ilijulikana pale Mombasa kuwa mwisho wa eneo la Mrima[2].
Marejeo
- ↑ Sensa ya 2012, Tanga - Pangani DC[dead link]
- ↑ Krapf aliandika katika kamusi yake: "MRIMA (ulio tini (chini) ya milima, ni Mrima, si kisiwa), a tract of country beginning with Oassi (Wasini) and stretching as far as the Pangani River and Kipumbui (Kipumbwi)"
![]() |
Kata za Wilaya ya Pangani - Mkoa wa Tanga - Tanzania | ![]() | ||
---|---|---|---|---|
Bushiri | Bweni | Kimang'a | Kipumbwi | Madanga | Mkunguni | Mkalamo (Pangani) | Mkwaja | Mwera | Pangani Magharibi | Pangani Mashariki | Tungamaa | Ubangaa
|