Mwera (Pangani)
Mandhari
Mwera ni kata ya Wilaya ya Pangani katika Mkoa wa Tanga, Tanzania, yenye Postikodi namba 21304.
Kata ya Mwera ina vijiji vitatu ambavyo ni Mwera, Ushongo na Mzambarauni.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 6,059 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 4,601 waishio humo.
Wakazi wa kata hiyo wanajihusisha na shughuli mbalimbali kama vile uvuvi katika bahari ya Hindi, ambayo inapatikana katika kijiji cha Ushogo, na kilimo cha mboga, ufuta, nyanya, mahindi, pia ni wafanyabiashara na wanafanya ujasiriamali mbalimbali.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Kata za Wilaya ya Pangani - Mkoa wa Tanga - Tanzania | ||||
---|---|---|---|---|
Bushiri | Bweni | Kimang'a | Kipumbwi | Madanga | Masaika | Mikunguni | Mkalamo | Mkwaja | Mwera | Pangani Magharibi | Pangani Mashariki | Tungamaa | Ubangaa
|