Nenda kwa yaliyomo

Mkoa wa Pangani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkoa III Pangani wakati wa koloni ya Kijerumani katika Tanzania (hadi mwaka 1918)
Historia ya Tanzania
Coat of Arms of Tanzania
This article is part of a series
Uendo
Historia ya Zanzibar
Afrika Mashariki 1800-1845
Ukoloni
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
Mkwawa
Vita vya Maji Maji
Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
Tanganyika
Mapambano ya uhuru Tanganyika
Uhuru
Uhuru wa Tanganyika
Mapinduzi ya Zanzibar
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Julius Nyerere
Ujamaa
Tamko la Arusha
Vita vya Kagera
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin Mkapa
Jakaya Kikwete
John Magufuli
Samia Suluhu Hassan

Tanzania Portal

Mkoa wa Pangani (kwa Kijerumani Bezirk Pangani) ulikuwa mkoa wa kihistoria katika koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ukahesabiwa kama mkoa wa tatu kati ya mikoa 24 ya koloni hilo lililojumlisha Tanzania bara, Rwanda na Burundi za kisasa.

Ofisi kuu ya Mkoa ilikuwako mjini Pangani na ofisi ndogo Handeni.

Mkoa ulikuwa na umbo la kanda lililoenea kutoka pwani ya Bahari Hindi kuelekea takriban kilomita 200 upande wa magharibi hadi milima ya Uluguru, wenye upana kati ya kilomita 60 na 80.

Maeneo yake yalilingana takriban na wilaya za Pangani, Handeni na Kilindi.

Mkoa wa kikoloni wa Pangani ulikuwa na eneo la km² 12,600.

Upande wa kusini ulipakana na mkoa wa Bagamoyo, upande wa kaskazini na mkoa wa Tanga na upande wa magharibi na mkoa wa Kondoa-Irangi. Mpaka wa kusini ulifuata mwendo wa mto Mligasi. Mto mkubwa katikati ya mkoa ulikuwa mto Msangasi.

Mwaka 1913 waliishi humo Waafrika 98,500 waliokuwa pamoja na wafanyakazi 6,000 waliohamia hapa kwa kazi ya mashamba makubwa kutoka sehemu nyingine, Wazungu 123 na wakazi "wenye rangi" (maana yake watu wasiokuwa Waafrika wala Wazungu) 1814.

Katika kilimo watu wengi walilima kwa ajili ya mahitaji yao lakini Wazungu kadhaa walianzisha mashamba makubwa baada ya Waarabu waliowahi kuwa na mashamba yaliyolimwa na watumwa karibu na miji ya Pwani.

Mwaka 1913 kampuni 13 na walowezi 16 walilima hasa mkonge na mpira na maeneo ya mashamba haya ya Kizungu yalikuwa takriban km² 500. Mashamba hayo kulikuwa na ajira kwa wafanyakazi kutoka nje ya mkoa.

Mifugo ilikuwa kazi ya Waafrika. Serikali ilihesabu mwaka 1913: