Kamusi ya Koloni za Kijerumani (1920)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

"Deutsches Kolonial-Lexikon" ni jina la Kijerumani la "Kamusi ya Kikoloni ya Kijerumani" iliyotolewa mwaka 1920. Kamusi hii ilikusanya habari juu ya koloni zote za Ujerumani kabla ya 1914.

Kamusi imepita kipindi cha hakimiliki ikawekwa mtandaoni kama programu huria. Ni rejeo muhimu la habari za kihistoria kuhusu nchi zilizokuwa chini ya Ujerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kama vile Tanzania, Rwanda, Burundi, Kenya (Witu), Namibia, Togo na Kamerun barani Afrika na maeneo ya Pasifiki kama Samoa, Guinea Mpya na visiwa vya Mariani halafu Tsingtao (Uchina).

Kamusi iliandikwa kwa lugha ya Kijerumani na wataalamu wa jiografia, biolojia, uchumi, lugha na masomo mengi mengine wenye ujuzi kuhusu nchi walioeleza katika kamusi. Kuna takwimu nyingi katika makala za kamusi hii.

Katika mambo ya utamaduni na historia inapaswa kusoma makala yake kiangilifu. Mara nyingi itikadi ya ubaguzi wa rangi iko wazi kabisa pia udharau kwa wenyeji katika koloni hizi. Lakini hata hivyo mwanahistoria ataitumia kama kumbukumbu muhimu.

Kamusi ilikuwa tayari 1914 lakini haikuchapishwa kwa sababu ya vita. Kuchapishwa kulitokea baada ya vita tu. Mhariri alikuwa Heinrich Schnee aliyewahi kuwa gavana wa mwisho wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Deutsches Kolonial-Lexikon / hrsg. von Heinrich Schnee. - Leipzig : Quelle & Meyer 1920. - 3 Bde.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Kamusi inapatikana mtandaoni kwenye anwani: Deutsches Koloniallexikon