Pangani (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Pangani
Skyline ya Pangani
Pangani is located in Tanzania
Pangani
Pangani
Mahali pa mji wa Pangani katika Tanzania
Anwani ya kijiografia: 5°24′36″S 38°58′48″E / 5.41°S 38.98°E / -5.41; 38.98
Nchi Tanzania
Mkoa Tanga
Wilaya Pangani
Pangani - Boma la Kale

Pangani ni mji wa Tanzania uliopo ufukoni mwa Bahari Hindi kati ya Dar es Salaam na Tanga ukielekea pande zote mbili za mdomo wa mto Pangani. Leo hii ni mji mdogo mwenye wakazi karibu 8000 na makao makuu ya Wilaya ya Pangani. Lakini ina historia ndefu hasa kwa sababu kuna bandari nzuri ya kiasili mdomoni wa mto wa Pangani inayofaa jahazi ndogo.

Majengo mbalimbali ya kale ni ishara ya historia ndefu ya mji huu. Pamoja na Boma, lililojengwa na Waarabu wa Unguja na kutumiwa na wakoloni wa Kijerumani na wa Kiingereza, kuna nyumba za Waswahili.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kuna uwezekano ya kwamba Pangani ina historia ya miaka 2000. Hii inategemea kama kweli Pangani ni sawa na mji wa Rhapta unaojulikana kutokana na kitabu cha Periplus ya Bahari ya Eritrea kilichoandikwa mnamo mwaka 70 B.K. Walakini siku hizi wataalam wa akeolojia wanaamini kuwa Rhapta ilikuwepo kwenye sehemu nyingine ya pwani ya Afrika ya Mashariki.

Pangani ilikuwa mji muhimu katika utamaduni wa Waswahili. Katika karne ya 19 BK iliona maendeleo chini ya utawala wa Zanzibar pamoja na miji mingine Uswahilini. Makabaila walilima miwa wakitumia kazi ya watumwa. Pangani ilikuwa pia kituo muhimu cha misafara iliyoanza hapa kuelekea ndani ya bara na pia soko muhimu la watumwa.

Mwanzo wa ukoloni Pangani ilikuwa mahali palipoanzia vita vya Bushiri mwaka 1889 dhidi ya utawala wa Wajerumani (Wajerumani). Mwakilishi wa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki Emil von Zelewski alimtendea liwali wa Sultani kwa ukali uliosababisha ghasia ya watu wa Pangani na kuanzisha Vita ya Abushiri. Baada ya kukomeshwa kwa vita hii umuhimu wa Pangani ulipungua sana kwa sababu Wajerumani walikazia maendeleo ya Tanga. Pia bandari ya Pangani hakufaa tena kupokea meli kubwa.

Polepole Pangani imerudi nyuma. Uhaba wa mawasiliano na barabara uliongeza mwendo huu. Hadi leo hakuna barabara ya lami kabisa katika wilaya yake.

Miaka ya nyumba mahoteli mbalimbali katika mazingira ya Pangani yameanza kutumia nafasi nzuri kwa utalii mwambaoni.