Nenda kwa yaliyomo

Mbuga za Taifa la Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa mbuga za taifa nchini Tanzania.
Mahali pa mbuga za taifa nchini Tanzania.

Mbuga za Taifa za Tanzania[1] ni nyingi tena mbalimbali, zikishika karibu theluthi moja ya eneo lote la nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Zinagawanyika kati ya:

  • Hifadhi za Taifa,
  • Hifadhi Teule,
  • Hifadhi ya Mawindo na
  • Mapori ya Akiba.

Hifadhi za taifa[hariri | hariri chanzo]

Hii ni orodha ya Hifadhi za Taifa, ambazo ni 19:

Hifadhi za Taifa Kiingereza Mkoa
Hifadhi ya Arusha Arusha NP Arusha
Hifadhi ya Burigi-Chato Burigi-Chato NP Kagera, Geita
Hifadhi ya Gombe Gombe Stream NP Kigoma
Hifadhi ya Ibanda-Kyerwa Ibanda-Kyerwa NP Kagera
Hifadhi ya Katavi Katavi NP Simiyu
Hifadhi ya kisiwa cha Rubondo Rubondo Island NP Mwanza
Hifadhi ya kisiwa cha Saanane Saanane Island NP Mwanza
Hifadhi ya Kitulo Kitulo Plateau NP Njombe
Hifadhi ya Mikumi Mikumi NP Morogoro
Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro Mount Kilimanjaro NP Kilimanjaro
Hifadhi ya Milima ya Mahale Mahale Mountains NP Kigoma
Hifadhi ya Milima ya Udzungwa Udzungwa Mountains NP Iringa, Morogoro
Hifadhi ya Mkomazi Mkomazi NP Kilimanjaro, Tanga
Hifadhi ya Ruaha Ruaha NP Iringa
Hifadhi ya Rumanyika-Karagwe Rumanyika-Karagwe NP Kagera
Hifadhi ya Saadani Saadani NP Pwani
Hifadhi ya Serengeti Serengeti NP Mara
Hifadhi ya Tarangire Tarangire NP Manyara
Hifadhi ya Ziwa Manyara Lake Manyara NP Manyara

Hakuna budi kuweka ulinzi mbugani kwani kuna majangili wanaoua ovyo wanyama kama vile tembo na kifaru: wanyama hao wanaweza kusaidia katika kuinua pato la taifa kupitia utalii.

Hifadhi za bahari na maeneo tengefu[hariri | hariri chanzo]

Ni mpango wa kimataifa kuwa asilimia 10 ya maji ya bahari na maziwa yawe chini ya hifadhi, na Tanzania ina asilimia 4.5 tu ya hifadhi ambayo inahusisha hifadhi za bahari 3 na maeneo tengefu 15.

Hifadhi za bahari[hariri | hariri chanzo]

Hifadhi ya kisiwa cha Mbudya, Dar es Salaam.

Hifadhi ya Bahari ni eneo kubwa ambalo hata watu wanaishi ndani yake. Shughuli za eneo hilo husimamiwa na Mpango wa Usimamiaji ujulikanao kama General Management Plan, ambao maandalizi yake yanashirikisha wadau woteː wanaoishi ndani ya hifadhi, Halmashauri husika ambazo ziko ndani ya hifadhi, na wengineo wakiwa ni pamoja na wanasayansi. Yanafanyika makubaliano ya kuwa baadhi ya maeneo yatengwe kabisa ambapo hakuna uvuvi wowote utakaoruhusiwa, kutenga maeneo ya matumizi ya jumla ambapo uvuvi unaruhusiwa kwa wavuvi wa ndani na nje ya hifadhi na maeneo ya matumizi maalum ambayo pamoja na kwamba wavuvi wa ndani ya hifadhi wanaruhusiwa kuvua kwa kutumia zana maalumu zinazokubalika, wavuvi wa nje hawaruhusiwi kabisa kuvua katika maeneo hayo.

Maeneo tengefu[hariri | hariri chanzo]

Kisiwa cha Bongoyo

Maeneo tengefu ni maeneo madogomadogo ya visiwa ambayo yanazungukwa na matumbawe. Katika maeneo hayo watu hawaruhusiwi kuishi wala matumizi ya rasilimali hayaruhusiwi. Shughuli zinazoruhusiwa katika maeneo hayo ni zile zinazohusiana na utalii tu. Maeneo hayo ni pamoja na visiwa vya Bongoyo na Mbudya mjini Dar es Salaam ambapo ndani yake kitengo kimetengeneza njia vinjari (nature trails) kwa ajili ya watalii kupita.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. ["TANAPA, Tanapa Brocha (Kiingereza)" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2012-09-20. Iliwekwa mnamo 2009-08-10. TANAPA, Tanapa Brocha (Kiingereza)]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: