Nenda kwa yaliyomo

Wilaya ya Mkuranga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Mkuranga (kijani cheusi) katika mkoa wa Pwani.

Wilaya ya Mkuranga ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Pwani.

Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 187,428 [1]. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 533,033 [2].

Eneo[hariri | hariri chanzo]

Wilaya hii ilianzishwa mwaka 1995 kutokana na maeneo ya wilaya ya Kisarawe. Eneo lake ni km² 2,432 na kuna pwani ya Bahari Hindi yenye urefu wa kilomita 90. Vijiji saba viko kando ya pwani, navyo ni Hungubweni, Mpafu, Kerekese, Kisiju Pwani, Mdimni, Magawa na Kifumangao. Vijiji vya Boza, Kuruti, Kwale na Koma viko kwenye visiwa vidogo baharini, si mbali na pwani.

Kuna misitu ya mikoko na wanyama walio hatarini kuangamizwa bado wana hifadhi hapa.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Wenyeji ni hasa Wazaramo, Wandengereko, Wamatumbi and Wamakonde.

Wakazi wa wilaya hukalia kata 25 zenye vijiji 120. Walio wengi (zaidi ya 90%) hudumisha maisha yao kwa njia ya kilimo hasa kilimo cha muhogo, mpunga na maharagwe. Mazao ya biashara ni korosho, nazi, mananasi na machungwa. Eneo hili ilikuwa kitovu cha kilimo cha korosho Tanzania takriban hektari 35,000 ilitumiwa kwa zao hili lakini tangu miaka ya 70 kilimo kilianza kupungua.

Wakazi wa vijiji vya pwani wanavua samaki.

Watu walio wengi ni maskini na utafiti wa mwaka 2005 ulionyesha kuwa familia ya wastani yenye watu 4.5 ilikuwa na pato la TSh 600,000 kwa mwaka (sawa na dola za Marekani 600) yaani chini ya dola 150 kwa mwaka kwa kila mtu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Mkuranga - Mkoa wa Pwani - Tanzania

Beta | Bupu | Dondo | Kimanzichana | Kiparang'anda | Kisegese | Kisiju | Kitomondo | Lukanga | Magawa | Mbezi | Mipeko | Mkamba | Mkuranga | Msonga | Mwandege | Mwarusembe | Njianne | Nyamato | Panzuo | Shungubweni | Tambani | Tengelea | Vianzi | Vikindu


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Pwani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Mkuranga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.