Kisiju
Kisiju ni kata ya Wilaya ya Mkuranga katika Mkoa wa Pwani, Tanzania yenye postikodi namba 61513 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,113 [2] walioishi humo.
Biashara na mawasiliano[hariri | hariri chanzo]
Kitovu chake ni mji mdogo ambao ni ni bandari kwenye pwani la Bahari Hindi na kisiwa cha Kwale inahesabiwa ndani ya eneo lake. Kisiju iko takriban kilomita 100 kusini ya Dar es Salaam upande wa kaskazini wa delta ya mto Rufiji.
Eneo la mji mwenyewe lina takriban hektari 8. Ni bandari kubwa kati ya Dar es Salaam na Kilwa. Biashara yote kutoka na kwenda visiwa vya Kwale na Koma inapita bandari yake pamoja na sehemu za bidhaa zinezopelekwa Mafia. Kuna huduma ya mabasi kwenda Dar es Salaam.
Historia[hariri | hariri chanzo]
Eneo la Kisiju pamoja na visiwa limekaliwa tangu zamani sana. Wataalamu wa akiolojia waligundua mabaki ya makazi ya kibinadamu tangu karne ya 1 BK [3]
Mabaki ya bidhaa yamepatikana tangu karne ya 6 na hii inadokeza kuwa eneo la Kisiju lilikuwa kwenye vituo vya kwanza vya biashara ya pwani iliyokuwa chanzo cha utamaduni wa Uswahilini
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ https://www.tcra.go.tz/images/documents/postcode/pwani.pdf[dead link]
- ↑ Sensa ya 2012, Pwani - Mkuranga DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-06-10.
- ↑ Archaeological Work at Kisiju,Tanzania, 1994 - taarifa ya F. Chami and E. T. Kessy. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-03-14. Iliwekwa mnamo 2009-03-04.
![]() |
Kata za Wilaya ya Mkuranga - Mkoa wa Pwani - Tanzania | ![]() |
---|---|---|
Beta | Bupu | Dondo | Kimanzichana | Kiparang'anda | Kisegese | Kisiju | Kitomondo | Lukanga | Magawa | Mbezi | Mipeko | Mkamba | Mkuranga | Msonga | Mwalusembe | Mwandege | Njia nne | Nyamato | Panzuo | Shungubweni | Tambani | Tengelea | Vianzi | Vikindu |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Pwani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kisiju kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |