Mkoa wa Singida

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mahali pa Mkoa wa Singida katika Tanzania.

Mkoa wa Singida ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania ukipakana na mikoa ya Arusha, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tabora na Shinyanga. msimbo wa posta ni 43000[1]

Kuna wilaya sita za Iramba, Manyoni, Singida Vijijini na Singida Mjini, Ikungi na Mkalama. Wakati wa sensa ya mwaka 2012 jumla ya wakazi ilikuwa 1,370,637 [2].

Wakazi wa wilaya za Singida mjini na kijijini ni hasa Wanyaturu. Walio wengi Iramba ndio Wanyiramba na wakiwa Wagogo wengi huko Manyoni.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Singida ni kati ya maeneo maskini zaidi ya Tanzania. Uchumi wake ni hasa ufugaji: idadi ya ng'ombe hukadiriwa kuwa takribani milioni 1.4. Masoko hayako karibu na barabara si nzuri.

Kilimo si kizuri kwa sababu ya hali ya mvua. Ukame huleta njaa. Singida ni kati ya mikoa inayotegemea misaada ya chakula.

Pamoja na kuwa mkoa wa Singida umekuwa ukikumbwa na njaa kwa sababu ya ukame, na hata pale mvua inaponyesha ni duni sana, una shughuli mbalimbali ambazo zinaingiza kipato kwa watu wa mkoa huo.

Ikiwa kuanzia miaka ya 1990 na kuendelea mpaka sasa imekuwa madini ya dhahabu yakigunduliwa katika sehemu mbalimbali mkoani Singida japo kumekuwa aidha hakufanyiwi uchunguzi wa kina kuhakiki kiwango cha hifadhi ya madini iliyopo katika eneo husika au huwa kiwako kilichopo ni kidogo, hivyo kutokuvutia wawekezaji wakubwa katika maeneo hayo. Kati ya madini ambayo yamewahi kugunduliwa katika mkoa wa Singida ni dhahabu ambayo imewahi kugunduliwa huko Londoni na Iruma wilayani Manyoni.

Majimbo ya bunge[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]


 
Mikoa ya Tanzania
Bandera Tanzania
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi