Wanyaturu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Wanyaturu (au Waturu; wao hupendelea kuitwa Arimi, yaani watu wa Rimi) ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Singida.

Lugha yao ni Kinyaturu, ambacho ni jamii ya Kibantu, lakini kina fonimu nyingi za Kikushi.

Asili ya kabila hilo inasemekana ni nchi ya Ethiopia ambako kunasadikiwa kuwa na kabila wanaotumia lugha ambayo kwa asilimia kubwa inafanana na Kinyaturu. Hudhaniwa pia kuwa Wanyaturu na WakushI wa Ethiopia asili yao ni moja.

Pengine jina "Wanyaturu" linapoteza historia yao kwani liliundwa na Wazungu.

Walipoingia eneo la Tanganyika walichangamana na Wanyatunzu pamoja na Wasukuma, ndiyo maana mila na tamaduni zao zinashabihiana kwa kiasi kikubwa, hivi kwamba ni vigumu kumpambanua Mnyaturu baina ya Wanyatunzu.

Wana utani na Wanyiramba na Wairaqw.

Mwaka 1993 walikuwa 556,000 [1].

Ndani ya kabila hilo, kuna makundi matatu: Vahi (Wahi), ambao ni zaidi ya nusu ya Wanyaturu wote, na kuwa wenyeji wa mji wa Singida: Hawa wanaishi kuanzia Singida mjini hadi karibu ya wilaya ya Manyoni; Airwana (Wilwana) wanaishi kaskazini kwa ziwa Singida; na lile dogo zaidi la Anyiŋanyi (Wanyinganyi) wanaishi maeneo ya Mnying'anyi. [1]

Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wanyaturu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. Unaweza kubadilisha hapa kuhusu airwana kuwa si wengi karibu nusu ya Wanyaturu wote kwa ukianzia pale mjini Singida ukielekea Kusini hadi sehemu za Issuna hadi Itigi na Manyoni hadi Kintinku hawa ni Vahi tu, bado sijasema sehemu za Ihanja hadi Muhintiri na sehemu za Mang'onyi na Misughaa ni vahi au wahi kwa hiyo robo tatu ya wanyaturu ni wahi yaani vahi waweza kufanya utafiti na utagundua ukweli huo. wairwana wana maeneo kuelekea Kaskazini ambayo nisehemu fupi au ndogo sana kiieneo na inapakana na wanyiramba ukifika sehemu za Iguguno.