Wangindo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Wangindo ni kabila la watu wanaoishi Kusini mwa Tanzania, katika wilaya ya Liwale, mkoa wa Lindi.

Lugha yao ni Kingindo.

Wangindo walikuwa warushamishale maarufu na wazuri na walitumiwa sana, hasa na chifu wa Wahehe Mkwawa alipokuwa akipambana na Wabena na Wasangu.

Wangindo, mbali ya kuishi kusini mwa Tanzania, pia wameenea katika sehemu tofautitofauti za nchi, zikiwemo Zanzibar, Morogoro na Mbeya (katika kijiji cha Rujewa ambacho inasemekana walipewa na Mkwawa baada ya kumsaidia katika vita.

Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wangindo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.