Nenda kwa yaliyomo

Wadatoga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wadatooga)
Wadatoga wakiwamba ngozi.

Wadatooga (pia huitwa Wataturu au Wamang'ati) ni kabila la watu wa Kiniloti nchini Tanzania wanaoishi hasa katika mikoa ya Manyara, Mara, Arusha, Singida, wachache pia Tabora, Simiyu na Shinyanga[1].

Wataturu wanaopatikana mikoa hiyo lugha yao ni moja, Kidatooga, ingawa lahaja zake zinatofautiana [2] kiasi kwa kufanya maelewano kuwa magumu. Ila wale wanaopatikana nje ya mikoa hiyo ni jamii nyingine.

Mwaka 2000 walikadiriwa kuwa 87,978.[3]

Kuna walau makundi saba:

  • Wabajuta
  • Gisamjanga (Kisamajeng, Gisamjang)
  • Wabarabayiiga (Barabaig, Barabayga, Barabaik, Barbaig)
  • Waasimjeeg (Tsimajeega, Isimijeega)
  • Warootigaanga (Rotigenga, Rotigeenga)
  • Waburaadiiga (Buradiga, Bureadiga)
  • Wabianjiida (Biyanjiida, Utatu)

Watani wa Wataturu ni Wasukuma na Wamasai, ingawa mwanzoni walikuwa wanaogopwa sana na Wamasai.

Desturi ya Wataturu ni kuoa wake wengi na kuwa na utajiri wa mifugo. Jamii hiyo inategemea sana mifugo. Kilimo ni kwa sehemu ndogo sana.

Wataturu ni watu wakarimu sana na hufanya kazi kwa umoja na si vinginevyo.

Wanaume hunyoa vipara kwa sehemu ya kichwa ila wanawake hufuga nywele zenye urembo, tofauti na Wamang'ati [4].

Miundo ya kucheza ngoma ni miundo ya kushikana mikono au kucheza kwa duara.

Wanaume hufanyiwa tohara kwa kisu bila ganzi; kisu hicho hupitishwa kwenye moto ili kuzuia damu kuvuja baada ya kukata. Huacha kimshipa chini kikiwa kinaning'inia kwa kuamini kwamba huleta ladha kipindi cha kujamiana.

Tiba za asili ndiyo kitu pekee wanachokitumia. Pia ni jamii ambayo hujihusisha na kuunga mifupa.

  1. https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/wadatooga-wizi-na-kugombea-mwanamke-kwao-ufahari-4860018
  2. Wataturu husalimia kwa kuanza na neno, seyu!? Ila Wamang'ati husema Seyi!? Huu ni moja ya tofauti kilahaja.
  3. [1]
  4. Baadhi ya jamii hufananisha Wataturu na Wamasai au Wamang'ati ila wenyewe WAnajuana kimavazi na kimazungumzo.
Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wadatoga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.