Wangulu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Wangulu (au Wanguu) ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi mipakani mwa mikoa minne ya Tanga, Dodoma, Manyara na Morogoro, hasa upande wa Kusini-Magharibi mwa mkoa wa Tanga ambako sasa ni wilaya ya Kilindi na upande wa Kaskazini-Mashariki mwa mkoa wa Morogoro ambako sasa ni wilaya ya Mvomero. Upande wa Magharibi ni mkoa wa Manyara ambayo sasa ni wilaya ya Kiteto.

Masimulizi ya kale ya Mbega na Kimweri yanasema kuwa kabila hili la Wanguu ndilo kabila mama la makabila ya Wazigua, Wabondei, Wasambaa, Waluvu na Wakilindi, ambapo makabila hayo yanaendeleza mila na desturi za asili moja na katika umoja huo hujulikana pia kwa jina moja la Waseuta.

Mwaka 1987 walikuwa 132,000 hivi.[1]

Ungulu na chanzo cha ukoloni[hariri | hariri chanzo]

Historia ya Tanzania
Coat of Arms of Tanzania
This article is part of a series
Uendo
Historia ya Zanzibar
Ukoloni
Mgawanyo wa Afrika
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
Mkwawa
Vita vya Maji Maji
Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
Tanganyika
Uhuru
Mapinduzi ya Zanzibar
Julius Nyerere
Ujamaa
Tamko la Arusha
Vita vya Kagera
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin Mkapa
Jakaya Kikwete
{Kigezo:Data99

Tanzania Portal

Eeno la Wangulu lilijulikana kwa jina ya "Nguru / Ngulu au kama inavyojulikana kwa siku hizi Nguu" kwa Wajerumani wakati wa ukoloni.

Ndiko mkoloni Mjerumani Karl Peters alifanya mkataba wa kwanza kwa maeneo yaliyokuwa baadaye koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Peters aliyekuwa ameondoka Saadani, alifika Nguru 23 Novemba 1884 [2] alipokutana na mmoja Masungu [3] Biniani.

Kufuatana na maelezo ya Peters, huyu alikuwa "Sultani wa Nguru" aliyefanya urafiki naye, baadaye aliweka alama yake kwenye karatasi iliyoandikwa na Peters na wenzake. Katika matini iliyopelekwa baadaye Berlin, mji mkuu wa Ujerumani, Masungu Binani kama Bwana wa "nchi za Katungekaniani na Kwindokaniani katika Nguru" alikubali kukabidhi haki zote za kiutawala na wa kiuchumi kwa Shirika la Ukoloni wa Kijerumani lililowakilishwa na Peters.

Kuna wasiwasi mwingi kama huyu Biniani alikuwa chifu au sultani wa eneo gani, pia kuna mashaka kama alielewa walau punje karatasi ilisema nini na kama alama ni kweli yake.

Hivyo ndivyo pia kuhusu "mikataba" mingine ya Peters. Lakini karatasi hizo zilitosha kuweka msingi kwa ukoloni wa baadaye.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Ethnologue report for language code: heh. Ethnologue.com. Iliwekwa mnamo 2013-02-02.
  2. kufuatana na Jutta Bückendorf: "Schwarz-weiss-rot über Ostafrika !" uk 202 hii ilitokea huko Mkindo, Hembeti, lakini mkataba wenyewe unataja "Quatunge Quaniani" na "Kwindokaniani" kama mahali pa kutia sahihi.
  3. pia: "Mafungu"
Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wangulu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.