Wabende

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wabende ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Katavi na Mkoa wa Kigoma, katika Wilaya ya Uvinza na Wilaya ya Mpanda. Kwa mkoa wa Kigoma hujulikana haswa kama Watongwe, wanapatikana haswa katika wilaya ya Uvinza kwa maeneo ya Uvinza, Ilagala, Mgambazi, Rukoma, Igalula, Mgambo, Buhingu, Katumbi, Kalya, Kashagulu na Sibwesa na kujichukulia umaarufu sana kwa jimbo la Kigoma kusini na kuitwa Tongwe. Ingawa wilaya ya Uvinza ukiwatafuta kwa jina la Wabende itakuwa vigumu lakini hawajatofautiana kwa mila, desturi, lugha na [[utamaduni] pia.

Mwaka 1999 idadi ya Wabende ilikadiriwa kuwa 27,000 [1], lakini takwimu ya mwaka 2016 inakadiria watu 125,000.

Lugha yao ni Kitongwe. Husalimiana kwa kupiga magoti na kupiga makofi, huku wanatamka maneno "nandamsya tata" ikiwa anayesalimiwa ni baba, au "nandamsya majo" ikiwa ni mama.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wabende kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.