Wakwere

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Wakwere (pia wanaitwa Wanghwele) ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi hasa katika Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. Wanakadiriwa kuwa zaidi ya laki moja.

Lugha yao ni Kikwere.

Kama Waluguru, Wakaguru, Wakutu na Wazaramo, kabila hilo linafuata mfumojike, yaani ukoo wa mama ndio unaoongoza familia na watoto wote wanahesabiwa kuwa wa ukoo huo.

Baadhi ya sifa zao ni kuwa watu wastaarabu, wanakirimu sana wageni; Wakwere huona fahari pale ambapo nyumba yao imejaa wageni.

Pia Wakwere hawana chifu kama makabila mengine ila wana msemi ambaye ndiye kiongozi mkubwa kwenye jamii yao. Mfano ni Kikwete na Kidanga.

Mwisho, Wakwere wengi ni watawala yaani viongozi.

Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakwere kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.