Waalagwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wasi (au Waalagwa) ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Dodoma, Wilaya ya Kondoa, hasa tarafa ya Kolo katika vijiji kama Kwa Dinu, Mneniya, Hurui n.k. Watu hao wapo pia mkoani Manyara (Babati mjini na Galapo). Kati ya makabila yaliyopo Kondoa linaweza kuwa kabila la pili kwa ukubwa na wingi baada ya Warangi.

Lugha yao ni Algwaisa si Chasi ambayo ni mojawapo ya lugha za Kiafrika-Kiasia, si ya Kibantu, kwani huendana na Kifyomi, Kiiraqw na Kiburunge ambazo zote hizi ni lugha za Kikushi. Kabila hili sehemu zote wanazokaa wenyewe huongea lugha hii na ndiyo asili yao ya wazazi wao waliowakuta.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Katika tarafa ya Kolo kulikuwa na mmiliki aliyeitwa sultani Salim Kimolo (toka enzi za ukoloni). Sultani huyo alikuwa anaongea sana lugha hiyo, ukizingatia yeye alikuwa mtu kama jamii ya Wamang'ati au Wairaqw. Alipofika Kondoa - Kolo na lugha hiyo ilipochukua nafasi akapaita Kolo kama Kolowasi. Alikuwa na watoto 43, na watu wote walimuheshimu na kutumia lugha hiyo hata katika kutoa maamuzi wakati wa kesi mbalimbali. Watu wengi wa jamii hii ni Waislamu kutokana na mahusiano kati ya sultani Salim Kimolo na Waarabu hapo zamani.

Watu wamestaarabika, ni wakulima na wafugaji.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waalagwa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.