Babati Mjini
Babati | |
Mahali pa mji wa Babati katika Tanzania |
|
Majiranukta: 4°13′12″S 35°45′0″E / 4.22000°S 35.75000°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Manyara |
Wilaya | Wilaya ya Babati Mjini |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 93,108 |
Babati ni mji mdogo mwenye halmashauri na hivyo hadhi ya wilaya katika Mkoa wa Manyara nchini Tanzania yenye postikodi namba 27100[1] . Ni pia makao makuu ya Mkoa wa Manyara, takriban kilomita 170 kusini mwa Arusha na kilomita 220 upande wa kaskazini mwa Dodoma. Mji uko karibu na Mbuga wa Tarangire ukienea kati ya ncha ya kaskazini ya Ziwa la Babati na karibu na tako la Mlima Kwaraa (2145 m juu ya UB).
Hadi mwaka 2012 kata za mji wa babati zilikuwa sehemu ya Wilaya ya Babati ya awali; baadaye Babati Mjini na Wilaya ya Babati Vijijini zilitengwa kuwa halmashauri mbili za pekee.
Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, wilaya hii ya Babati mjini ilikuwa na wakazi wapatao 93,108 waishio humo. Kata iliyopo kitovu cha mji huitwa pia "Babati" ikiwa na wakazi 16,718.[2]
Babati iliendelea kiasi kutokana na kukaa kando la barabara kuu kati ya Dodoma na Arusha. Hata hivyo ilikuwa kama kijiji kikubwa tu hadi kuwa makao makuu ya Wilaya ya Babati iliyoanzishwa mwaka 1985. Tangu siku zile iliendelea kukua haraka hadi kupata halmashauri yake kama mji na kuwa mji mkuu wa mkoa mpya mwaka 2012.
Tangu kutengenezwa kwa barabara kuu watalii wameanza kufika Babati.
Asili ya jina Babati[hariri | hariri chanzo]
Kuna hadithi inayosimuliwa kuhusu asili ya jina. Zamani za ukoloni wa Kijerumani barabara ilijengwa karibu na mahali pa Babati ya leo. Msimamizi Mjerumani akamwauliza kijana mwenyeji je jina la mahali ni nini? Lakini kijana hakumwelewa akafikiri huyu mgeni aliuliza eti babake ni nani. Hivyo akamjibu kwa lugha ya Kigorowa "baba ti" inayomaannisha "baba ni huyu" akimdokezea mzee aliyekaa karibu. Mjerumani alifikii hii ni jina akaiandika ikabaki hadi leo.[3]
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ https://www.tcra.go.tz/images/documents/postcode/manyara.pdf[dead link]
- ↑ Sensa ya 2012, Manyara Region – Babati Town-Council
- ↑ Haya ndiyo maelezo aliyosikia mwanahabari huko Babati, taz. Babati a town with intriguing history, Sosthenes Mwita in 28 September 2015 Daily News Archived 9 Oktoba 2015 at the Wayback Machine.
Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]
- KEFW Babati Link Group website Archived 28 Septemba 2007 at the Wayback Machine.
- Babati a town with intriguing history, Sosthenes Mwita in 28 September 2015 Daily News Archived 9 Oktoba 2015 at the Wayback Machine. (iliangaliwa 23-10-2015
![]() |
Kata za Wilaya ya Babati Mjini - Mkoa wa Manyara - Tanzania | ![]() |
---|---|---|
Babati | Bagara | Bonga | Maisaka | Mutuka | Nangara | Sigino | Singe |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Babati Mjini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |