Dodoma (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Jiji la Dodoma
Mji wa Dodoma
Mji wa Dodoma
Anwani ya kijiografia: 6°10′S 35°44′E / 6.167°S 35.733°E / -6.167; 35.733
Nchi Tanzania
Mkoa Dodoma
Idadi ya wakazi (2012)
 - 2,083,588

Dodoma ni mji wa Tanzania ya kati. Imetangazwa kuwa mji mkuu wa Tanzania mwaka 1973. Hali halisi makao ya kikazi ya serikali ya Tanzania yako Dar Es Salaam pia ikulu halisi ya rais. Lakini bunge hukutana Dodoma na sehemu za ofisi za wizara kadhaa zimepelekwa Dodoma. Mji ni pia makao makuu ya Mkoa wa Dodoma na eneo lake inahesabiwa kama Wilaya ya Dodoma.

Eneo la mji liko 1135 m juu ya UB. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, mji wa Dodoma ilikuwa na wakazi wapatao 410,956 [1] waishio humo.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Kiuchumi ni kitovu cha biashara ya kilimo cha karanga, maharagwe, alizeti na mizabibu, pamoja na mifugo na kuku.

Dodoma kuna makao makuu ya Kanisa la Biblia Publishers pamoja na Emmaus Shule ya Biblia.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Elimu inahitaji kuboreshwa, hasa maeneo ya vijijini, maana ndio mji mkuu: hivyo kunahitajika kuboreshwe zaidi.

Mawasiliano[hariri | hariri chanzo]

Mawasiliano ni mazuri kwa barabara ya lami kuanzia mji wa Dodoma kwenda Morogoro - Dar Es Salaam au Morogoro - Iringa, barabara zingine ni za udongo to pamoja na njia kuu kuelekea Tanzania ya Magharibi - Rwanda - Kongo. Pia hali ya barabara ya kale ya "Cape - Cairo" inayovuka Dodoma kutoka kaskazini (Arusha - Kondoa) kwenda kusini si nzuri tena. Kuna pia njia ya reli ya kati kutoka Dar Es Salaam kwenda Kigoma yenye matatizo ya mara kwa mara. Dodoma ina uwanja wa ndege wa kitaifa .

Asili ya jina[hariri | hariri chanzo]

Neno "Dodoma" linasemekana kumetokana na neno la kigogo "dodomia" kufuatili historia kwamba zamani kuna tembo alikuja pale mjini akakita nyayo zake ardhini akiacha alama ya nyayo zake zimedidimia.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Dodoma ilianzishwa wakati wa ukoloni wa Kijerumani kama kituo kwenye reli ya kati penye karahana ya reli. Tangu 1912 imekuwa makao makuu ya mkoa. 1913 Dodoma ilikuwa na posta, simu, hoteli na maduka 26 (moja ya mzungu, mengine ya Wahindi na Waarabu). Kikosi cha polisi kilikuwa na askari 59.

Dodoma imeendelea kuwa mji mdogo mpaka kutangazwa kuwa mji mkuu. Azimio hili lilileta ujenzi na maofisi kadhaa ya serikali. Kwa ujumla uhamisho unaendelea kuchelewa kwa sababu mbalimbali; sababu muhimu ni ya kwamba watumishi wa serikali na wanasiasa walio wengi hawapendi kuondoka katika jiji halisi na kuhamia mji mdogo ambao ni mbali sana na mazingira waliyoyazoea. Menginevyo kuna matatizo ya kifedha ambayo yamesaidia haidi sasa kutangaza nia ya kuhami lakini kubaki palepale.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Dodoma mjini - Mkoa wa Dodoma - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Chahwa | Chamwino | Chang'ombe | Chigongwe | Chihanga | Dodoma Makulu | Hazina | Hombolo | Ipagala | Ipala | Iyumbu | Kikombo | Kikuyu Kaskazini | Kikuyu Kusini | Kilimani | Kiwanja cha Ndege | Kizota | Madukani | Majengo | Makole | Makutupora | Mbabala | Mbalawala | Miyuji | Mkonze | Mnadani | Mpunguzi | Msalato | Mtumba | Nala | Ng'hong'honha | Ntyuka | Nzuguni | Tambukareli | Uhuru | Viwandani | Zuzu

  1. Sensa ya 2012, Dodoma - Dodoma MC