Iringa (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Iringa
Skyline ya Iringa
Iringa is located in Tanzania
Iringa
Iringa
Mahali pa mji wa Iringa katika Tanzania
Majiranukta: 7°46′12″S 35°41′24″E / 7.77°S 35.69°E / -7.77; 35.69
Nchi Tanzania
Mkoa Iringa
Wilaya Iringa Mjini
Idadi ya wakazi
 - 112,900
Iringa, 1906

Iringa ni mji mkubwa katika kusini ya Tanzania mwenye hadhi ya manisipaa. Ni makao makuu ya Mkoa wa Iringa na eneo lake ni wilaya ya Iringa mjini. Idadi ya wakazi ni mnamo 112,000.

Asili ya jina la Iringa ni neno la Kihehe "liliga" lenye maana ya boma. Mji umejengwa juu ya mlima ukitazama mto Ruaha bondeni.

Mji uko kanda la barabara kuu ya TANZAM kuna usafiri wa kila siku kwenda Dar es Salaam na Mbeya. Njia kwenda Dodoma ni sehemu ya barabara ya kale ya "Cape-Cairo" kati ya Rasi ya Afrika Kusini na Kairo wa Misri lakini kwa sasa ni barabara ya udongo tu.

Kuna viwanda mbalimbali, hospitali, chuo kikuu na ofisi kuu za dayosisi za kanisa katoliki, Waluteri (KKKT) na Waanglikana.

Iringa ilianzishwa mwaka 1892 kama kambi la jeshi la kikoloni wakati wa vita ya Wajerumani dhidi ya Wahehe. Mji wa leo upo mahali pa "Neu Iringa" au Iringa mpya ya Wajerumani waliotumia jina hili baada ya kuharibu boma la mtemi Mkwawa huko Kalenga waliloita "Iringa" tar. 31 Oktoba 1894.


Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Iringa mjini - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Gangilonga | Ilala] | Isakalilo | Kihesa | Kitanzini | Kitwiru | Kwakilosa | Makorongoni | Mivinjeni | Mkwawa | Mlandege | Mshindo | Mtwivila | Mwangata | Nduli (Iringa mjini) | Ruaha