Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka KKKT)
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
Mkuu wa kanisa: Askofu Dk. Fredrick Onael Shoo
Uhusiano: All Africa Conference of Churches (AACC)
Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)
World Lutheran Federation
Idadi ya dayosisi: 20
Wanachama: Milioni 6,1
Anuani ya barua: P.O. Box 3033
Arusha, Tanzania
Tovuti rasmi: http://www.elct.org/

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ni muungano wa Kilutheri katika nchi ya Tanzania.

Mwaka 1938 makanisa saba ya Kilutheri yaliungana kama Muungano wa Makanisa ya Kilutheri, na tarehe 19 Juni 1963 yalikuwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.[1]

Lengo la KKKT ni kuwapa watu nafasi ya kumfahamu Yesu Kristo ili kupata uzima wa milele. Kanisa limejengwa juu ya msingi wa Yesu Kristo, linaongozwa na Neno la Mungu kama linavyopatikana katika Agano la Kale na Agano Jipya (Biblia ya Kikristo), na limeimarishwa katika sakramenti.

KKKT linaongozwa na Mkuu wa kanisa (Askofu Mkuu) na maaskofu ishirini na nne kutoka dayosisi ishirini na nne, wakiwa na wanachama zaidi ya milioni 6,3 wanaolifanya kuwa la pili duniani kati ya makanisa ya Kilutheri (baada ya lile la Uswidi).

Ofisi kuu ya KKKT iko katika mji wa Arusha.

KKKT lina uhusiano na All Africa Conference of Churches (AACC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Lutheran World Federation (LWF) na Lutheran Mission Cooperation (LMC).

KKKT ni chama kinachowapa wanachama chake nafasi ya kumwabudu Mungu, kupata elimu ya Kikristo na huduma nyingi nyingine.

Matawi[hariri | hariri chanzo]

  • Elimu (Sekondari and Chuo Kikuu)
  • Fedha na Utawala
  • Afya na Utibabu (Mahospitali 21 na zahanati nyingi)
  • Umisheni na Uinjilisti
  • Upangaji na Maendeleo
  • Hudumu ya Jamii na Kazi ya Akinamama

Dayosisi[hariri | hariri chanzo]

  • Dodoma
  • Iringa
  • Kati
  • Kaskazini
  • Kaskazini-Kati
  • Kaskazini-Mashariki[2]
  • Kaskazini-Magharibi[3]
  • Karagwe
  • Konde
  • Kusini
  • Kusini-Kati
  • Kusini-Magharibi
  • Kusini-Mashariki
  • Kusini-Mashariki kwa Ziwa Viktoria
  • Mashariki ya Ziwa Viktoria
  • Mashariki na Pwani
  • Mara
  • Mbulu
  • Meru
  • Morogoro
  • Pare
  • Ruvuma
  • Ulanga Kilombero
  • Ziwa Tanganyika

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Homepage. Evangelical Lutheran Church in Tanzania (2007). Iliwekwa mnamo 2008-12-17.
  2. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2017-03-25. Iliwekwa mnamo 2010-09-12.
  3. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-03-02. Iliwekwa mnamo 2010-09-12.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]