Ruaha Mkuu
Ruaha Mkuu (pia: Ruaha Mkubwa) ni mto muhimu nchini Tanzania na tawimto la Rufiji. Huitwa "Ruaha Mkuu" kwa kuutofautisha na "Ruaha Mdogo" unaoishia ndani yake, si mbali na Iringa Mjini.
Jina Ruaha kwa Kihehe linamaanisha "maji mengi".
Chanzo na mwendo wa mto
[hariri | hariri chanzo]Chanzo chake ni mito mingi midogo inayotelemka milima ya nyanda za juu za kusini mwa Tanzania, hasa safu za milima ya Uporoto na ya Kipengere. Mito hii inakusanya maji yake kwenye tambarare ya Usangu na ndipo Ruaha inapoanza. Mito mikubwa zaidi inayoungana hapa na kuunda Ruaha ni pamoja na mto Mbarali, mto Kimani na mto Chimala.
Karibu na Ng’iriama mto unatoka katika Usangu na kuingia hifadhi ya kitaifa ya Ruaha. Inaendelea kupokea Ruaha Mdogo na mto Kisigo kabla ya kuingia katika ziwa la lambo la Mtera, halafu inaendelea hadi lambo la Kidatu.
Baada ya Kidatu, Ruaha Mkuu unapita tambarare ya Kilombero hadi kuishia katika mto Rufiji.
Matatizo ya ekolojia ya mto
[hariri | hariri chanzo]Maji ya Ruaha Mkuu ni muhimu kwa ekolojia ya beseni lake pamoja na watu wote wanaoishi huko. Lakini matumizi ya binadamu yameleta mvurugo kwa ekolojia ya mto na tangu mwaka 1993 mto umeanza kukauka wakati wa ukame. Uhaba wa maji umesababishwa na matumizi mabaya ya maji upande wa miradi mikubwa ya mpunga katika Usangu.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Mito ya Tanzania
- Orodha ya mito ya mkoa wa Mbeya
- Orodha ya mito ya mkoa wa Iringa
- Orodha ya mito ya mkoa wa Morogoro
- Orodha ya mito ya mkoa wa Pwani
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Geonames.org
- WWF.org - The Ruaha Water Programme Archived 15 Machi 2007 at the Wayback Machine.
- Ruaha information with images Archived 9 Oktoba 2006 at the Wayback Machine.
- FAO review
- FAO - fact sheet on the ecohydrology of the Great Ruaha River (2003) Archived 11 Juni 2007 at the Wayback Machine.
- Öhman, May-Britt, Taming Exotic Beauties: Swedish Hydro Power Constructions in Tanzania in the Era of Development Assistance, 1960s - 1990s, Stockholm, 2007, PhD Thesis
7°56′S 37°52′E / 7.933°S 37.867°E
Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ruaha Mkuu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |