Mto Wami

Majiranukta: 6°7′S 38°49′E / 6.117°S 38.817°E / -6.117; 38.817
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

6°7′S 38°49′E / 6.117°S 38.817°E / -6.117; 38.817

Mto Wami.
Daraja la Wami karibu na Mandera (A 14) lililojengwa mwaka 1960.

Mto Wami ni mto wa Tanzania mashariki, unaotiririka katika mkoa wa Morogoro hadi mkoa wa Pwani.

Chanzo chake ni katika Milima ya Ukaguru na unaishia katika Bahari Hindi magharibi kwa Zanzibar.

Beseni lake ni kubwa: km² 43,946[1].

Matawimto yake ni Mto Mkata upande wa kushoto na Mto Lukigura, Mto Mjonga na Mto Chogoati upande wa kulia.

Njia yake inaanza katika Hifadhi ya Mikumi, unakata barabara ya B 129 takriban kilomita 42 kutoka Morogoro. Unaendelea kuelekea mashariki ukipita barabara ya A 14 karibu na Mandera, unaendelea kupita Mvomero na kuishia baharini.

Mto huo umepita katika eneo la kambi ya magereza Mbigiri katika Dakawa. Huo mto husifika sana kwa uvuvi katika eneo hilo la Dakawa. Lakini huo mto unajulikana pia kwa kuwa na mamba wengi pamoja na viboko wakubwa.

Baadhi ya watu hutumia maji hayo kwa kunywa, kuogea, kufulia, kupikia pamoja na shughuli nyingine.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa karne ya 19 mto Wami ulikuwa njia mojawapo ambako misafara kutoka pwani ilielekea bara. Ni hasa misafara kutoka Saadani iliyotumia njia hii. Henry Morton Stanley alipita hapa alipomfuata Emin Pasha.

Mwaka 1884 Karl Peters na wenzake walitumia njia ya Wami walipoingia Tanganyika bara na kutembelea watawala wa kieneo waliotia sahihi kwenye mikataba iliyoweka chanzo cha kuunda koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.

Barabara kuu ya A14 kutoka Dar es Salaam na Chalinze kuelekea Moshi na Tanga inapita mto huo kwenye daraja jembamba lililojengwa mwaka 1960[2]. Daraja jipya linajengwa kando lake[3].

Kuna mipango ya kuongeza daraja lingine huko Gama (Mkange) kati ya Saadani na Bagamoyo kwa ajili ya barabara tarajiwa kati ya Mombasa na Dar es Salaam kufuatia mwambao wa Bahari ya Hindi[4].

Picha[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-09-01. Iliwekwa mnamo 2017-08-22. 
  2. CO 1069-164-22, picha ya daraja kutoka The National Archives UK, tovuti ya Flikr
  3. Wami Bridge reaches halfway to completion, gazeti la Guardian 28.04.2021
  4. ESIA summary for the proposed upgrading Tanga - Pangani - Saadani - Makurunge (229 km) road to bitumen standard in Tanga and Coast Regions, Tanzania, tovuti ya afdb.org

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]