Morogoro (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Jiji la Morogoro
Skyline ya Jiji la Morogoro
Jiji la Morogoro is located in Tanzania
Jiji la Morogoro
Jiji la Morogoro
Mahali pa mji wa Morogoro katika Tanzania
Anwani ya kijiografia: 6°49′12″S 37°39′36″E / 6.82°S 37.66°E / -6.82; 37.66
Nchi Tanzania
Mkoa Morogoro
Wilaya Morogoro Mjini
Idadi ya wakazi
 - 228,863
Morogoro mjini

Mji wa Morogoro ni mji nchini Tanzania uliopo takriban kilomita 200 upande wa magharibi wa Dar es Salaam ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Morogoro. Kulingana na sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 228,863 [1]

Mji uko kando ya milima ya Uluguru. Ni kitovu cha viwanda vya mazao na mahali pa Chuo Kikuu cha Sokoine. Morogoro ni mji ujulikanao kwa muziki wa kitanzania. Kwanza kabisa ilikuwa makao ya bendi marrufu ya Cuban marimba band chini ya mwanzilishi wake Salum Abdallah mzaliwa wa mji huo. Makao makuu ya bdeni hiyo yalikuwa Kichangani, mjini Morogo. Nyimbo za santuri nyingi za miaka ya 1950 na 1960 zilitungwa mjini humo. Mji huu ulikuwa ni makao ya bendi nyingine ya Moro jazz. Mwaka 1968, Mbaraka Mwinshehe mwana muziki mashuhuri wa Morogoro aliiwakirisha Tanzania kwenye maonyesho ya ulimwengu ya biashara yaliyokuwa mji wa Osaka, Japan, na baada ya kurudi kwake alitunga wimbo uliokuwa marrufu nchini wa maonyesho hayo. Mbaraka alifariki kwa ajali ya gari mjini Mombasa, Kenya. Mji wa Morogoro unajulikana kwa klabu za mchezo wa mpira. Wapenda mchezo huo watamkubuka mchezaji wa timu ya taifa Sembuli ambaye alikuwa mchezaji maarufu wa timu ya klabu ya Yanga. Morogoro ni njiapanda ya barabara muhimu za Dar es Salaam - Mbeya na Dar es Salaam - Dodoma zinazokutana hapa. Pana pia kituo cha reli ya kati kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, Mwanza na Kigoma. Reli ya TAZARA hupita nje ya mji mbali kidogo.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Morogoro (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: