Kingolwira
Kata ya Kingolwira | |
Majiranukta: 6°49′12″S 37°38′36″E / 6.82000°S 37.64333°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Morogoro |
Wilaya | Morogoro Mjini |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 15,823 |
Kingolwira ni kata ya Wilaya ya Morogoro Mjini katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania, yenye Postikodi namba 67119.
Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 21,953 waishio humo. [1] Hata hivyo, baada ya sensa, kata iligawanyika ili kuzaa kata mpya ya Tungi. Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 15,823 [2].
Wakazi wa Kingolwira wanajihusisha sana na shughuli za uchumi kama vile biashara, kilimo n.k.
Pia ni moja kati ya sehemu zilizojaliwa kwa uoto wa asili mzuri kama vile misitu, vichaka na milima mikubwa ya Uluguru yenye safu za kupendeza.
Makabila yapatikanayo huku ni Waluguru, Wasukuma, Wakwere n.k.
Mwaka 1971 Kingolwira ilikuwa mahali pa kambi ya wanajeshi kutoka Uganda waliowahi kukimbia utawala wa Idi Amin. Walikusanywa huko na rais aliyepinduliwa Milton Obote ambaye alifanya mipango ya kurudi Uganda tena kwa kibali cha Julius Nyerere. Kundi la askari 294 liliondoka tena kwenye Agosti 1971 wakielekea Tabora wakashiriki mwaka 1972 katika jaribio lililoshindikana la Obote kumwondoa Amin madarakani[3].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ http://www.meac.go.tz/sites/default/files/Statistics/Tanzania%20Population%20Census%202012.pdf Archived 2 Januari 2004 at the Wayback Machine. Wilaya ya Morogoro Mjini - Mkoa wa Morogoro
- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ David Martin, General Amin, London 1974, ISBN 0571105858, uk 171-174
Kata za Wilaya ya Morogoro Mjini - Mkoa wa Morogoro - Tanzania | ||
---|---|---|
Bigwa | Boma | Chamwino | Kauzeni | Kichangani | Kihonda | Kihonda Maghorofani | Kilakala | Kingo | Kingolwira | Kiwanja cha Ndege | Luhungo | Lukobe | Mafiga | Mafisa | Magadu | Mazimbu | Mbuyuni | Mindu | Mji Mkuu | Mji Mpya | Mkundi | Mlimani | Mwembesongo | Mzinga | Sabasaba | Sultan Area | Tungi | Uwanja wa Taifa |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kingolwira kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |