Idi Amin

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Idi Amin
Idi Amin pamoja na Askofu Luwum aliyeuawa baadaye kwa amri yake.
Idi Amin akibebwa kifalme na wafanyabiashara Waingereza huko Kampala.

Idi Amin Dada alikuwa rais wa Uganda tangu mwaka 1971 hadi 1979, alipofukuzwa na jeshi la Tanzania.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alikuwa mwanajeshi akapanda ngazi kuwa jenerali na mkuu wa jeshi la Uganda.

Mwaka 1971 alimpindua rais Milton Obote akajitangaza kuwa rais mpya, lakini wengine hawakumtaka.

Mara moja alianza kuwatesa wafuasi wa Obote na watu wote waliompinga. Kuna makadirio ya kwamba jumla ya watu 100,000 hadi 500,000 waliuawa katika miaka minane ya utawala wake.

Aliharibu uchumi wa Uganda kwa ufisadi na majaribio ya kuongoza biashara. Hatua kubwa ya uharibifu ilikuwa kufukuza watu wote wenye asili ya Kihindi na kugawa maduka na biashara yao kwa ndugu au wafuasi wa rais. Takriban watu 80,000 walipaswa kuondoka kwao wakihamia Uingereza, Marekani au Kanada hasa.

Mnamo Oktoba 1978 Amin alianzisha vita dhidi ya Tanzania kwa kuvamia sehemu za mkoa wa Kagera. Rais Julius Nyerere wa Tanzania aliamua kumwondoa Amin kabisa na jeshi la Tanzania likatwaa Kampala tarehe 11 Aprili 1979.

Amin alitorokea Libya, halafu Irak na mwishowe Saudia alikopewa kimbilio kwa masharti ya kutoshughulikia siasa tena.

Alikufa mjini Jeddah tarehe 16 Agosti 2003.

Administradors.png Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Idi Amin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.